Mchezaji wa Simba na timu ya Taifa ya Rwanda
kiungo mkabaji Patrick Mafisango amefariki dunia kwa ajali ya gari leo alfajiri
katika eneo la Tazara jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Simba
bwana Aden Rage amesema kuwa taarifa za awali juu ya chanzo cha kifo cha
mchezaji huyo zinasema kuwa mchezaji huyo amekutwa na mauti akiwa
anaendesha gari na kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki.
Msiba huu unakuja wakati kocha wa timu ya Taifa ya Rwanda Milutin Sredovic 'Micho' akiwa amemteuwa kepteni wa zamani wa timu hiyo Hamada Ndikumana a.k.a 'Katauti' na Patrick Mafisango kujiunga na timu ya taifa hilo (AMAVUBI) kwaajili ya maandalizi ya nchi zitakazofuzu kwenda Brazil kwenye michuano ya Kombe la dunia 2014.
Kabla ya kuichezea Simba mchezaji huyo alitokea Azam Fc ya jijini Dar es salaam.
Patrick Mafisango is dead.
Muweza twakuomba uilaze roho ya marehemu
Patrick Mafisango kulingana na maamuzi yako japo tunashauri umlaze pema peponi, Jah rasta farie.
No comments:
Post a Comment