Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA
mkoani Kagera Bwana WILFRED MUGANYIZI RWAKATARE, amewasihi wananchi
kutokumbatia maovu katika jamii.
Amesema kuwa kumekuwa na tabia ya watu kuwabeba wanoujumu
uchumi wa wenzao kwa kunufaisha familia zao, hivyo wananchi wametakiwa
kuwatambua na kuwa makini na watu hao.
Bwana Rwakatare, amesema kuwa kinapofika kipindi cha
uchaguzi wananchi wachague kwa umakini
kwa kufanya tathmini kujua ni
nani atawaletea maendeleo katika jamii, kwa kuhepusha kuwachagua watoa rushwa
kwani mleta maendeleo anaonekana.
Ameongeza kuwa maisha kwa sasa ni magumu hivyo jitihada za
wananchi ndizo zitanusuru taifa, hivyo waachane na hitikadi za vyama badala
yake washirikiane kujishughulisha na kuwafichua wanaosadikika kufuja fedha za
umma.
Hata hivyo Bwana Rwakatare amewakumbusha wananchi kushiriki
kikamilifu katika suala sense litakalofanyika mwezi wa nane mwaka huu, kwa
kuwataka wananchi kukubali kuhesabiwa sehemu yoyote watakayokuwa siku hiyo
kwani ni taratibu za nchi.
Sensa ya watu na makaazi inatarajiwa kufanyika usiku wa kuamkia Agost 25 mwaka huu,
limeshazinduliwa katika mikoa ya Tabora, Dar es salaam na Mbeya.
No comments:
Post a Comment