Tel. 255 022 2443205/2443286/2443450;
Mobile 255 0754 784050, 0715 784050; 0784 784050 Fax
255 022 2443244; Email info@tgnp.org ; web www.tgnp.org
16/05/2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TGNP kufanya mafunzo ya uraghibishi mikoa mitatu
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) utafanya mafunzo
ya uraghibishi ngazi ya jamii kwa mikoa
mitatu ya Shinyanga, Morogoro na Mbeya, ambapo
katika mikoa hiyo watajikita katika wilaya za Mbeya vijijini, Morogoro Vijijini na Kishapu. Mafunzo haya yataanza tarehe 22 – Mei
2011 – 2 June 2012.
Mafunzo hayo yana malengo ya kuwajengea wananchi
uwezo wa kushiriki, kuchambua kwa kina fursa na changamoto zinazowakabili katika
mazingira yao na kuyatafutia ufumbuzi
kwa kujenga vuguvugu la ukombozi wa wanawake kimapinduzi.
Matarajio ya matokeo makubwa ya Mafunzo ya Uraghibishi na utafiti shirikishi wa kijamii,yatawashirikisha
wanawake na wanaume walioko
pembezoni katika kutambua fursa
walizonazo katika kudai au kuingizwa kwa madai
yao katika mchakato wa Katiba mpya, kudai mabadiliko ya sera,
kimfumo, na haki ya uchumi kwa makundi
yaliyoko pembezoni.
Mafunzo haya pia yatawajengea wanajamii uwezo wa
kushiriki ipasavyo katika mchakato wa kutoa maoni kwa Tume ya Kuratibu Mchakato
wa katiba mpya, haki ya uchumi, na maisha endelevu kwa wote.
Imetolewa
na
Usu Mallya
Mkurugenzi
Mtendaji wa TGNP
No comments:
Post a Comment