Balozi Kagasheki ambaye pia ni mbunge jimbo la Bukoba mjini
CCM, amesema kuwa lazima masuala ya wananchi yasimamiwe kwa pamoja kwasababu
wanasiasa wanafuta dola na kuajiri watalaamu watekeleze mambo ya wananchi.
Amesema kuwa kujenga soko la kisasa ni muhimu lakini
wanatafuta sehemu pembezoni mwa mji ili kuupanua na watu wafanye biashara kwa
uhuru, uhalifu ulioibuka manispaa ya Bukoba amesema kuwa wanashirikiana na
kamanda wa polisi kuukomesha wanameshaweka mkakati mbadala lakini baadhi ya
wavunjifu wa amani wasitumie siasa kuhatarisha amani iliyopo...................
Kuhusu kubadilisha namba za pikipiki kupitia TRA, Balozi
Kagasheki amesema ni utaratibu muhimu wa serikali ambao hatahivyo tatizo
linatokea baada ya kukutwa pikipiki nyingi zina madeni hivyo jamii kujikuta
gharama ya kubadili inakuwa kubwa.
Hatahivyo amesema muda uliotolewa na mfupi lakini
akasisitiza kuwa wameongea na wabunge wengine na kumshawishi waziri wa fedha
ili atafute namna ya kuongeza muda jambo ambalo litapatiwa jibu hivi punde.
Ameongeza kuwa kumekuwa nchi kama Marekani rais akiondoka
madarakani na watendaji wote wa serikali wananondoka, hivyo watendaji wa Tanzania
wasiharibu kazi kwa kisingizio cha kuondoa vyama madarakani kwasababu wao
watasalia, kuwa hiyo ni kuwatesa wananchi.
Mbunge huyo amesema suala la viwanja tayari limeanza
kushughulikiwa na fidia zitarekebishwa kwa waliopimia, na hiyo imeanza mara
moja tangu katibu m,wenezi CCM taifa alipoondoka Bukoba.
Na mwisho amesema CCM ni ile ile, wananchi walewale na
mbunge ni Yule Yule, hivyo kugombea kuko palepale kwa lengo la maendeleo ya
wananchi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment