MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday 24 March 2015

ALICHOKIONA RAIS KIKWETE BAADA YA KUTEMBELEA WAHANGA 1500 WA MAFURIKO BUGURUNI HIKI HAPA

Rais Jakaya Kikwete amefanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Buguruni Mnyamani ili kujionea madhara makubwa ya mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam na kusababisha zaidi ya watu 1500 kukosa hifadhi baada ya nyumba zao kuingiwa na maji.

Baada ya Rais Kikwete kuwasili  katika eneo hilo amebaini tatizo kuwa linatokana na ukosekanaji wa mtaro wenye uwezowa kupitisha maji yanayozibwa na uchafu pamoja na ujenzi usiosalama................
 
Akizungumza na wakazi wa Buguruni Mnyamani,Rais Kikwete amesema amelazimika kufika katika eneo hilo ili kuona jitihada zinazofanyika za kuondoa maji hayo ili wananchi wawe salama huku akikisisitiza kuwa baada ya maji hayo kuondolewa, ujenzi wa bomba mpya ambao ni mkubwa ufanyike ili kusaidia kupitisha maji wakati wa mafuriko.
 
Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo akiwemo mzee Saidi Mohamed Bakari amesema wanaishi maisha ya tabu na wana siku saba hawajalala kutokana na maji hayo kuingia ndani ya nyumba zao.

Na Mwanaharakati.

No comments: