Kamanda Thobias Sedoyeka, amesema habari zinazoendelea kuruhswa leo katika mitandao na baadhi ya redio na Tv kama habari mpasuko, wananchi wazipuuze kwani ni ajali iliyotokea januari mwaka jana.
Awali zimesambazwa habari kuwa ................
Abiria 13 wakiwamo watatu wa familia moja wamefariki
mkoani Singida leo, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongwa na Lori
Scania leo saa moja na nusu asubuhi katika barabara ya Singida Dodoma, katika
kijiji cha Isuna.
Kamanda wa polisi mkoani Singida sacp Geofrey Kamwela amesema gari hiyo ni
Noah T 730 BUK ambapo amesema miili10 tayari imeshatambuliwa na ndugu na jamaa,
na watatu bado kutambuliwa na imefadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti katika
hospitali ya mkoa wa Singida. Endelea kufuatilia tutakuletea undani.
Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu Kamanda amesema kuwa vyombo hivyo hivyo vilivyotangaza habari hiyo awali virudie kuikanusha kwani siyo ya kweli.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment