Diwani kata Kagondo manispaa ya Bukoba, ambaye hatahivyo
alikuwa meya wa manispaa ya Bukoba Anatory Aman, amezomewa na wananchi baada ya
kuitisha mkutano wa hadhara kuzungumzia matatizo ya maji yanayowakabili
wananchi wa kata hiyo.
Katika mkutano huo, Mh Aman alitaka kujua undani wa matatizo
ya maji yanayowakabili wananchi hao, ambao hatahivyo wameshalalamika zaidi ya
mwaka sasa, tangu kujengewa kwa vyanzo mbalimbali vya maji na kusababisha
ukosefu mkubwa wa maji kwa wananchi hao....................
Wananchi wameanza kumzomea diwani huyo, kwakusema kuwa yeye
hafai kuwaongoza kutokana na kushindwa kuitisha mkutano hata mmoja, tangu
achaguliwe kuwa diwani wa kata hiyo kwenye uchaguzi mwaka 2010.
Siku chache zilizopita, wananchi wa mtaa wa Kagondo
Karuguru, alitoa malalamiko yao kuhusu vyanzo hivyo vya maji kupitia vyombo vya
habari, ambapo katika mkutano huo, diwani wao alitaka kuwaeleza jinsi
alivyoweka mpango wa kupeleka wataalamu ili watoe ushauri na kushughulikia
tatizo hilo, ambalo limetokana na kujengewa kwa vyanzo vya asili vya maji
ambavyo baada ya kujengewa kwa sementi na kuwekewa mabomba, maji yameonekana
kukauka kama siyokuziba.
Katika maelezo yao wananchi, vyanzo hivyo vilijengewa na
TASAF mwanzoni mwa mwaka jana, ambapo vilifanya kazi kwa muda wa wiki mbili tu.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment