Bwana HassahMwambene akiongea na waandishi habari |
Kubadilika kwa teknolojia na hali
halisi ya maisha, kumebadilisha tasnia ya habari hivyo kuwalazimu waadishi wa habari
wabadilike kulingana na hali hiyo.
Akizungumza na waandishi wa mjini
Dodoma, mkurugenzi wa habari maelezo Bwana Hassah Mwambene, amesema kuwa
wanahabari waende sambamba na wanaowahabarisha kwa kuwapa habari zilizo sahihi
na zenye kuleta mabadiliko.
Bwana Mwambene amefafanua kuwa
matumizi ya mtandao kihabari yanakuwa makubwa zaidi kwasasa, huku akiongeza
kuwa kuna kila sababu ya kuweka utaratibu maalumu kuwezesha watumiaji kuweka
habari zenye tija kwani watakuwa wakifuatiliwa na kusimamiwa na mamlaka.
Amesema ukishakuwa mwanahabari, unatakiwa
kuchambua mambo mambo buhimu kuwekwa kwenye chombo husika, kwa kuvaa
viatu vya Yule anayeandikwa au kutangazwa kama umemtendea vyema au vibaya, huku
akitolea mfano picha za utupu na sura za watu zinazowekwa na baadhi ya wamiliki
wa mitandao kwa udhalilishaji.
Amesisitiza kuwa Tanzania imekuwa na
baadhi ya wadau wanaojidhalilisha na kuingiza mijada kati ya Tanzania na
mataifa mengine, kwasababu ya watanzania kubeza mambo yaliyopo nchini badala ya
kutafuta jinsi ya kurekebisha.
Waandishi habari 20 kutoka kanda
mbalimbali wanaounda mtandao wa SAUTI, wanaendelea na mafunzo ya kuandika na
kutangaza habari kupitia mtandao, yaliyodhaminiwa na mfuko wa waandishi wa
habari Tanzania TMF, ambapo pia wanajadili jinsi ya uendelezaji wa taasisi ya
SAUTI kwa lengo la kuwafikia wanyonge na kuleta sauti zao adharani.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment