MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday 24 March 2015

NDEGE ILIYOANGUKA, KISANDUKU CHA KUMBUKUMBU CHAPATIKANA

Ni ndege ya abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Germanwing Airbus A320 Imeanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa. 

Ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 142, wahudumu 6 na marubani 2ikitoka Barcelona Uhispania kuelekea Duesseldorf.

Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa chini ya nembo Germanwings imeripotiwa kuanguka karibu na mji wa Digne.

Ndege hiyo ya A320 ilianguka saa tano asubuhi katika Kusini mwa Milima ya Alps.
Viongozi wa Ujerumani na Ufaransa wanaendelea kushauriana kuhusiana na mkasa huo unaowakabilia macho.

Ndege hiyo ya Ujerumani imeanguka katika eneo lisilo na mijengo ambalo halifikiki kwa urahisi nchini Ufaransa Kusini mwa Milima ya Alps.

Taarifa inasema kisanduku cha kumbukumbu kimepatikana na kinaendelea kuchunguzwa ili kujua kamahali mbaya ya hewa ndiyo imesababisha ajali hiyo au vinginevyo.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametaja ajali hiyo kama mkasa na amesema kuwa uwezekano wa kuwapata watu wakiwa hai ni mgumu.

Hali ya hewa katika eneo hilo ilitajwa kuwa nzuri na kituo maalumu cha kukabiliana na mikasa kimetengwa kukabiliana na mkasa huo.

Waziri wa Maswala ya ndani ya nchi uko njiani kuelekea mahali pa ajali hiyo.
Vyombo vya habari nchini Ufaransa vinasema kuwa ndege hiyo ilituma ujumbe wa kuwa hatarini kabla ya mawasiliano yake kutoweka .

Na Mwanaharakati.

No comments: