MWENYEKITI
wa Kamati ya Shule ya Msingi Udasi mwambao mwa Ziwa Tanganyika, kata ya
Kabwe wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Ismail Ndomboya (42) amenusurika
kuuawa na mamba kwa kupambana kijasiri na mnyama huyo kwa zaidi ya nusu
saa.
Hata hivyo, licha ya kuokoa maisha yake mnyama huyo katika mapambano
hayo alimng’ata na kumnyofoa mkono wake wa kulia na kutokomea nao
ziwani...............
Diwani wa Kata ya Kabwe, Asante Lugwisha akizungumza na mwandishi wa
habari hizi kwa njia ya siku alithibitisha kutokea kwa mkasa huo
uliotokea juzi saa moja na nusu jioni wakati Ismail alipokuwa akioga
katika Ziwa Tanganyika kijijini Kabwe.
Akisimulia mkasa huo , Diwani Lugwisha alibainisha kuwa jioni hiyo ya
tukio Ismail aliamua kwenda kuoga ziwani wakati huo akiwa pekee ndipo
ghafla mamba alimvamia ghfla na kumuuma mkono wake wa kulia.
“Kwa ujasiri mkubwa Ismail alipambana kufa au kupona na mnyama huyo
kwa nusu saa huku akipiga yowe akiomba msaada lakini hakuna
aliyejitokeza kumsaidia kwa sababu sehemu aliyokuwa akioga ilikuwa mbali
na makazi ya watu,“ alieleza.
Aliendelea kueleza kuwa hatimaye mamba aliunyofoa mkono wa kushoto wa
Ismail na kutokomea nao ziwani ndipo Ismail alipokimbia kuelekea
nyumbani kwake akiwa uchi.
“Baadaye nilitaarifiwa kuwa Ismail ameshambuliwa na mamba wakati
akioga ndipo nilipofika nyumbani kwake, na tulijipanga tukamkimbiza
katika Hospitali Teule ya Wilaya (DDH) mjini Namanyere ambao tulifika
saa nne na nusu usiku ambako amelazwa kwa matibabu “ alieleza.
Mtaalamu wa afya wa Hospitali ya Wilaya, ambaye alikiri kuwa si
msemaji, alikiri kupokelewa kwa mgonjwa huyo aliyejeruhiwa na mamba
ambapo aliielezea hali yake kuwa inaendelea vizuri.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda amethibitisha
kutokea kwa mkasa huo na kwamba uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment