MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 16 March 2015

UAMUZI WA ZITTO KABWE AKIWA JIMBONI KWAO KIGOMA KASKAZINI JANA HUU HAPA

Wakazi wengi katika jimbo la Kigoma Kaskazini walikusanyika kumsikiliza Mbunge huyo na ujumbe wake aliosema awali kuwa wamuunge mkono kwa maamuzi atakayochukua, ambapo yeye Zitto Kabwe ambaye siku ya jana ameamua kuitumia rasmi kama kuwaaga wananchi  na wapiga kura wa jimbo lake.

Ijumaa ya wiki hii kupitia mtandao wa kijamii kwenye akaunti yake ya Twitter aliweka ujumbe kuwa hatogombea tena Ubunge kwenye uchaguzi ujao..................


Pamoja na kuomba kuungwa mkono, wananchi hawajamuunga mkono kwa uamuzi huo wa Mbunge wao Zitto Kabwe wa kutogombea tena ubunge.


Chadema ilimvua Zitto uanachama saa chache baada ya Mahakama Kuu kutupa shauri lake alilofungua akitaka chombo hicho cha sheria kimlazimishe katibu mkuu wa chama hicho kumpa nyaraka za mwenendo wa vikao vya Kamati Kuu vilivyomvua nyadhifa zote, huku akifanikiwa kupata amri ya muda ya kuizuia Chadema kumjadili.
Na Mwanaharakati.

No comments: