MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday 31 July 2014

MASIKINI NDOA YA MSANII MAARUFU LUCY KOMBA! MANENO YA KUPIMA UKIMWI YAANZA KUJITOKEZA

 
 Taarifa zinasema akiwa kwenye vikao vya maandalizi ya harusi na Mzungu, staa wa filamu Bongo, Lucy Francis Komba (pichani na mchumba wake), amejikuta katika wakati mgumu baada ya habari kudai kwamba, mchumba wake huyo amemwambia ili ndoa ifungwe lazima aoneshe cheti cha kipimo cha Ukimwi kwanza.
Chanzo chetu, kilisema kwa sasa Lucy anahaha kutafuta cheti feki cha kipimo hicho kwa kwenda hospitali mbalimbali ili anunue kwa gharama yoyote lakini imeshindikana.

“Ukweli Lucy anahaha kutafuta cheti cha Ukimwi, mchumba anasubiri akione vinginevyo hawatafunga ndoa,” kilisema chanzo.
 Ilidaiwa kuwa, mpaka sasa Lucy ameshafika kwenye hospitali tatu kubwa mbili, TMJ na Marie Stopes ili kufanya maarifa lakini imeshindikana.

Baada ya kupata habari hizo paparazi wetu alimtafuta Lucy ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Si kweli! Hao wanaosema hivyo ni wanafiki, sijui wanataka nini maana kila siku wanazusha mambo ya ajabu. Kwanza mimi huwa sitibiwagi kwenye hospitali hizo ulizozisema, natibiwa Regency.

“Kuhusu  kupima Ukimwi, mimi na mchumba wangu tulishapima hukohuko kwao Ulaya (Denmark) ndiyo maana tukaanza taratibu za ndoa.

“Namshangaa sana huyo aliyesema hayo hata kama ni mtu wangu wa karibu, mimi huwa simwelezi mtu mambo yangu binafsi kwa sababu duniani hakuna rafiki wa kweli, rafiki anakuchekea machoni lakini wote ni wabaya,” alisema Lucy.

taarifa za hospitali zinasema, hakuna utaratibu wa kumtaja jina mgonjwa kama alikwenda kutibiwa.

Na Mwanaharakati.

No comments: