Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma
salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Dkt. Parseko V. Ole
Kone kuomboleza kifo cha aliyepata kuwa Naibu Waziri, Mbunge na Katibu Mkuu wa
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Mheshimiwa Alhaji Mahami Rajab Kundya.
Mzee
Kundya aliaga dunia jana, Jumapili, Julai 27, 2014 mjini Zanzibar.
Katika
salamu zake, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa taifa
limempoteza Mzee Kundya katika kipindi ambacho ushauri wake ulikuwa unahitajika
sana na kuwa Watanzania wataendelea kumkumbuka kwa mchango wake katika nafasi
zote alizozishikilia za Serikali, za Chama cha Mapinduzi na za kidini.
“Naungana
nawe na wana-Singida wote katika kuomboleza kifo cha Mzee Kundya.Tumepoteza
kiongozi ambaye mchango wake utaendelea kukumbukwa na sisi sote. Kupitia kwako,
natuma pia salamu zangu za rambirambi kwa familia ya marehemu. Niko nao katika
kuomboleza msiba huu mkubwa na naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu
aiweke peponi roho ya Marehemu Mzee Kundya,”
amesema Rais Kikwete.
Imetolewa
na;
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
28
Julai,2014
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment