MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 31 October 2012

MECHI KATI YA TOTO AFRIKA NA KAGERA IMEAHIRISHWA SABABU YA MVUA NA WATU WATATU WAMENUSURIKA KIFO BAADA YA JIWE KUBWA KUPOROMOKA KUTOKA MLIMANI MKOANI MWANZA.

Watu watatu akiwemo mtoto mdogo wamekimbizwa hospitali ya mkoa Sekou Toure mara baada ya kuumizwa vibaya kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao kupitia jiwe lililoporomoka kutoka mlimani jijini Mwanza.

Waliokumbwa na ajali hiyo ni Bw. Msalam Husein(30) ambaye ni  dereva  na mkewe Bi. Nadia Grecian(25) ambaye ni mama wa nyumbani  pamoja na kichanga wao Asfati Mslam (aliyechini ya umri wa mwaka).


Tukio hilo limetokea leo hii majira ya saa 6:00 mchana katika nyumba wanayoishi kilima cha Sabato mtaa wa Ngara eneo la Mlimani B Kirumba jijini Mwanza ambapo pamoja na kwamba ni majira ya mchana watu hao  mke na mume walikuwa wamejipumzisha kitandani, (yawezekana kutokana na hali ya hewa kwa mvua inayoendelea kunyesha leo tangu asubuhi hadi muda huu tunakupa taarifa) ndipo wakakutana na ajali hiyo.


Kwa mujibu wa  Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya Ilemela  (OC-CID) Afande Magesa amesema kuwa hali ya Msalam Husein ni mbaya kwani amekimbizwa hospitali akiwa ajitambui huku mkewe akiwa akilia kwa maumivu makali kufuatia ajali hiyo.


Taarifa ya tukio hilo ilichelewa kufika polisi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha lakini hata hivyo polisi walifika eneo la tukio na kutoa msaada kwa kuwakimbiza hospitalini wajeruhiwa hao.
HABARI KWA HISANI GSENGO

No comments: