MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 30 October 2012

MKUTANO WA TISA WA BUNGE KUANZA VIKAO LEO MJINI DODOMA, WAKATI HUO CHAGUZI MBALIMBALI ZIKIKAMILIKA, AMBAPO NAPE NNAUYE ALONGA JUU YA UCHAGUZI.

Tarehe 28/10/2012 kumefanyika uchaguzi mdogo katika kata 29 kwenye mikoa mbalimbali nchini. Kata hizi zilikuwa wazi kwa sababu mbalimbali, hivyo kwa mujibu wa sheria ililazimika kufanya uchaguzi mdogo kujaza nafasi wazi.

Ukiacha matukio kadhaa ya vurugu, maeneo mengi uchaguzi umeenda kwa utulivu. Chama Cha Mapinduzi kinawapongeza wote waliofanya uchaguzi kwa amani na utulivu, huo ndio utamaduni wa watanzania, kushindana bila kupigana.

Muhutasari wa matokeo ya jumla unaonyesha kuwa TLP wameshinda kata moja(1), CUF wameshinda kata moja(1), CHADEMA wameshinda kata 5 na CCM imeshinda kata ishirini na mbili(22).

Kwa matokeo haya ambayo kwakweli yanatafisiri pana sana hasa ikizingatiwa kuwa mgawanyo wa kata ulikuwa nchi nzima basi matokeo haya yanatoa ujumbe wa jinsi CCM inavyokubalika nchini kwasasa.


Na pia ni uthibitisho wa kile kilichoitwa M4C(movement for change) kwa Chadema kuwa ni kiini macho kisichokuwa na matunda chanya bali ni M4D ( movement for dealth). Na hii inatokana na aina ya siasa za hovyo zinazoambatana na operesheni hii. Bila shaka sauti ya Watanzania kwa aina hii ya siasa imesikika bila kumumunya maneno.

Aidha kwa upande mwingine siasa za uongo,uzushi na ulaghai zilizotumiwa na vyama vya upinzani hasa Dr. Slaa kwenye kampeni hizo imekidhalilisha chama hicho na kudhalilisha utu uzima wa Katibu Mkuu huyo wa Chadema.

Mfano mzuri ni pale ambapo Dr. Slaa bila ya soni alipoamua kumzushia Rais na Mwenyekiti wa CCM kuwa kasafiri mpaka China eti kwenda kumuokoa mwanae ambaye kwa madai ya Dk. Slaa alikamatwa na madawa ya kulevya nchini humo.

Bila aibu Dr. Slaa alizusha uongo huo Tabora kwa wapiga kura huku akijua kuwa ni uongo, lakini hata hivyo uongo huo hauna sehemu kwenye kampeni hizo za udiwani. Wananchi walitegemea kusikia namna ya kutatua kero zao badala yake wakashuhudia mtu mzima akizusha ujinga wa ajabu.

Uongo huu na mwingine mwingi unathibitisha kuwa Dr. Slaa anazeeka vibaya kwani kila anavyoongeza siku hamu na tamaa yake ya kusema uongo ili kujiongezea umaarufu na kujenga chuki kati ya watanzania inaongezeka sana. Hakika TAPELI HUYU WA KISIASA, LICHA YA KUZEEKA VIBAYA SASA ANACHANGANYIKIWA.

Naamini mzigo aliotwishwa na wenzake unamlemea sana, hivyo namshauri awaachie vijana wajaribu kukiokoa chama hicho kinachoporomoka kwa kasi, vinginevyo wana Chadema waanze kuandaa matanga kwa chama chao.

Ukitazama mgawanyo wa ushindi huu utagundua kuwa, pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa kwenda na kupiga kambi kanda ya ziwa ameambulia kata sifuri(0). Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa kutumia gari ya serikali alijikita kusini nako katoka kapa.

Nguvu iliyotumika kutoka kwa vyama vya upinzani hasa Chadema hailingani na ushindi walioupata. Wakati CCM ikiwa busy na chaguzi za ndani ya Chama wao wamezungusha viongozi wa kitaifa nchi nzima na matokeo ndio hayo.

Tunawashukuru sana Watanzania kokote nchini walioendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kuendelea kuwaongoza na kutekeleza ilani yetu. Tunawaahidi utumishi uliotukuka.

No comments: