Akiongea na waandishi wa habari mkoani Kagera, kamanda wa polisi
mkoani humo kamanda Philipo Kalangi amesema kuwa majambazi walio huawa ni
mioingoni mwa majambazi sugu ambao wamekuwa wakijiusisha na vitendo vya uhalifu
ndani na nje ya mkoa kagera.
Jeshi la polisi mkoa kagera limefanikiwa kuwaua majambazi
watatu huku wengine wawili wakifanikiwa kukimbia hatua iliyofikia kufuatia
opreisheni inayo endelea kufanywa na jeshi la polisi mkoani humu ikilenga
kuwatia mbaroni watu wanao jiusisha na vitendo vya ujambazi mkoani humo.Katika opreisheni hiyo kumekamatwa injini tanoza boti zenye thamani ya shilingi milioni ishirini bunduki tatu na risasi 25.
Pia jeshi hilo limekamata misokoto ya bangi na lita 120 za pombe aina ya gongo katika operesheni inayoendelea mkoani humo.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment