Ni Kanisa la Kigango cha KAHYOLO kata ya Mikoni Bukoba vijijini, ambapo kunafanyika ujenzi huo, ambao una miaka kadhaa na bado unaendelea, hivyo mbunge wa jimbo hilo JASSON RWEIKIZA alipotembelea eneo hilo kujionea shughuli zao za ujenzi, mwenyekiti wa kamati ya ujenzi alimtembeza akimsihi kuwasaidia.
Mbunge huyo alichangia bando ya mabati yenye thamani ya shilingi laki 3.5.Chini ni shule ya msingi iliyoko kwenye Kata ya KAIBANJA Bukoba vijijini ambayo iliezuliwa na upepo mwezi Oktober, hata hivyo ukarabati unaendelea ambapo pia mbunge huyo alichangia kiasi cha shilingi laki tatu na nusu, ili kuchangia nguvu za wananchi.
Bukoba vijijini kumekuwa na tabia ya wazazi na walezi kuchapwa viboko na mugambo wakiongozwa na watendaji pamoja na viongozi wengine wa vijiji, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limekuwa likiwaweka wananchi katika wakati mgumu, hivyo wananchi wakiona mchango huo wanajihisi kuwa wameona mlango wa mbinguni.
No comments:
Post a Comment