MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday 8 January 2013

MAGAZETI LEO

BARAZA la Vijana la Chadema (Bavicha), limesema limemvua uanachama Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo, Juliana Shonza baada ya kubainika alikuwa akifanya vikao vya siri kukisaliti chama hicho akishirikiana na viongozi wa CCM.
Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche alisema Shonza alikuwa akiwashawishi wenzake kuitisha mikutano na waaandishi wa habari kumkashifu Katibu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa.
“Aende CCM hapa tumemg’oa kwa sababu alikuwa kirusi hatari kwa chama, alikuwa Chadema huku akifanya kazi na CCM, tuna ushahidi wa picha, mikanda ya video na ujumbe wa simu za mikononi,” alisema Heche.
Licha ya kumfuta uanachama Shonza, baraza hilo pia limewavua uanachama Habib Machange aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Kibaha Mjini na Mtela Mwampamba aliyegombea ubunge Jimbo la Mbozi Mashariki.

                         



POLISI jijini Arusha imekamata shehena ya nyara za serikali zenye thamani ya mamilioni ya shilingi wakati huo zikiwa zimefungwa kwenye makasha.
Inasemekana yalikuwamo mafuvu ya samba, mamba, tembo na wanyama wengine wa porini pamoja na ngozi za chui mamba tembo na meno mawili ya tembo.
 NI KWA HISANI YA GAZETI LA HABARI LEO 




TUME ya Mabadiliko ya Katiba, jana ilianza kukusanya maoni ya vyama vya siasa katika mchakato wa Katiba Mpya, huku baadhi ya vyama hivyo vikitoa mapendekezo mbalimbali kuhusu suala la urais.
Vyama vilivyozungumzia urais katika mkutano huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam ni CCM, CUF na Chadema.
Taarifa za vyama hivyo zilipatikana baada ya wawakilishi wao kuwasilisha maoni kwenye tume hiyo katika mkutano wa ndani ambao waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuingia.

Wakati CCM ikitaka Katiba ijayo iruhusu mgombea binafsi, Chadema imependekeza Mtanzania yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 18 aruhusiwe kupiga kura na kugombea nafasi yeyote ya uongozi nchini. CUF imependekeza Muungano wa Mkataba.

Mwanasheria wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alisema chama hicho cha upinzani, kimependekeza Katiba Mpya imtambue mtu mwenye umri wa kuanzia miaka 18 kuwa ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa kushika nafasi yoyote ya uongozi nchini.

                           








TAARIFA ZINASEMA BUNDUKI ZIMESALIMISHWA
POLISI nchini wametangaza kupokea bunduki 439 na risasi 37 kutoka kwa watu waliozisalimisha kutokana na wito uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi mwezi mmoja uliopita kuwataka wenye silaha kinyume cha sheria wazisalimishe.
Miongoni mwa silaha zilizosalimishwa na watu hao ni pamoja na shortgun (29), gobore (352), SMG (11), Riffle (20), bastora (22), Airgun (1), Rocket launcher (2) na SAR (2).

Msemaji wa polisi , Advera Senso alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kwamba kupatikana kwa silaha hizo ni ushirikiano mzuri kati ya polisi na wananchi.
Senso alisema polisi wamejipanga kwa kufanya operesheni maalumu itakayoendeshwa nchi nzima kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola pamoja na raia wema ili kuwabaini na kuwakamata wale wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria.

Alisema operesheni hiyo itafanyika kutokana na kumalizika kwa muda maalumu alioutoa Waziri Nchimbi kwa watu wenye silaha kuzisalimisha bila masharti yoyote.

Hata hivyo taarifa ya Senso haikutaja ni lini operesheni ya kusaka bunduki itaanza nchini.
Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za mtu ama kikundi cha watu wanaosadikiwa kujihusisha na umiliki wa silaha isivyo halali au matukio ya uhalifu wa aina yoyote ile ili kuhakikisha uhalifu wa kutumia silaha unapungua.”

Senso alibainisha kwamba mtu yeyote atakayetoa taarifa za mafanikio zitakazowezesha kukamatwa kwa watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria watazawadiwa Sh100,000 kulingana na mafanikio ya taarifa aliyoitoa.

No comments: