Kwa mwaka huu pekee amabo una wiki ya pili sasa, wasanii wawili wameshaaga dunia.
Omari Omar ambaye ni msaanii wa miondoko ya Mnanda/Mchiriku, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua
kwa muda mrefu.
Habari zinasema kuwa, Omar Omar aliyetamba na nyimbo mbalimbali kama 'Kupata ni Majahariwa' alifariki nyumbani kwao Temeke, saa chache baada ya kurejeshwa toka hospitali ya temeke alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.
Taarifa hizo zinasema kuwa mara baada ya kurejea nyumbani, msanii huyo alizidiwa na hatimaye kufariki na kwamba msiba wake upo nyumbani kwao Temeke Mikoroshini kwa ajili ya mipango ya mazishi.
Msiba wa msanii huo umekuja siku chache baada ya tasnia ya sanaa na burudani kumpoteza Juma Kilowoko 'Sajuki' msanii nyota wa filamu aliyefariki pia kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya muda mrefu.
Amefanya kazi hiyo sambamba na wasanii wengine na waliopenda kumuiga kama Dogo Mfaume, Ferouz, Easy Man na wengine.
No comments:
Post a Comment