Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imetoa
wito kwa Umoja wa Mataifa kuichukulia hatua Rwanda, kwa madai ya
kusaidia waasi nchini Congo badala ya kumfuatilia mtu mmoja kama vile
kanali Sultani Makenga.
Waziri wa habari
wa serikali ya Congo amesema hayo siku moja baada ya Umoja wa Mataifa
na Marekani kutangaza vikwazo dhidi ya kiongozi wa waasi wa M23,
Jenerali Makenga, vikiwemo vya usafiri na kukamata mali yake.
No comments:
Post a Comment