Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanya msako wa nyumba kwa nyumba,
mtaa na maeneo yaliyoathirika kwa hofu ya vijana ambao ni vibaka maarufu kama
Mbwa mwitu au Panya Road. Msako huu uliofanyika ndani ya masaa 24 hadi
alfajiri ya tarehe 26/5/2014 kwa lengo la kuwaondolea hofu na uhalifu dhidi ya
makundi ya vijana wadogo wasio na ajira ambao uliibuka hivi karibuni.
Maeneo
yaliyoathirika ni Kigogo, Magomeni, Tabata, maeneo yote yanayozunguka mto
Msimbazi, maeneo ya Mbagala nk. Msako huu unaendelea kufanywa na askari
wa vikosi maalum ambao wamepewa kazi ya kuhakikisha kuwa vikundi hivyo
haviibuki tena na vinatokomezwaa kabisa kwa kuwakamata wale wote
wanaojihusisha na vitendo vya kuvamia kwa mkundi wananchi ambao hawana hatia
Kamishna
kova ambaye amezungumza na wanahabari muda mfupi uliopita
Kati
ya watuhumiwa 149 waliokamatwa mmoja amegundulika kuwa ni kiongozi aitwaye
ATHUMANI SAIDI miaka 20, Mkazi wa Kigogo na amekiri anaongoza kundi la watu
zaidi ya 15 ambao baadhi yao ni kati ya waliokamatwa.
Imegundulika pia kwamba vijana hawa wanatumia dawa za kulevya aina ya bangi na
wengine hujichoma sindano na kuwafanya iwe rahisi kujihusisha na matukio ya
uhalifu. Vijana hao hupenda kushiriki katika ngoma kama Mnanda, Mchiriku,
Kigodoro, Kanga moja nk. ambazo kwa kawaida huchezwa hadi usiku wa
manane.
Wakitoka katika ngoma hizo hujikusanya pamoja na kufanya matukio ya uporaji kwa
mtu wanayekutana naye, kufanya uvunjaji katika majumba na wakati mwingine wana
mtindo wa kugema mafuta ya diesel au petrol katika matanki ya malori
yanayosafirisha mafuta.
Operesheni kali inafanyika katika maficho ya wahalifu hao ikiwa ni pamoja na
daraja la River side, Kigogo darajani, Manzese, maeneo ya Tandale pamoja na
maeneo mengine ya maficho mkoa wa Kipolisi Temeke.
Tunawasiliana na Maafisa utamaduni wa Wilaya zote za Mkoa wa D’Salaam
kusimamisha utoaji wa vibali wa ngoma za usiku ambazo hazina tija. Pia
Jeshi la Polisi linafuatilia na kuwavizia vijana wanaopora watu wanaotoka
katika sherehe za usiku kama vile Harusi na wanaotoka katika mikesha ya Ibada
na sehemu zozote zenye mikusanyiko.
Aidha Jeshi la Polisi wanapambana na vijana wanaowavizia watu katika vituo vya
mabasi pindi wanapotoka alfajiri kwenda katika shughuli zao za kila siku.
Zipo
taarifa kwamba baadhi ya wazazi wasio waaminifu wamewasafirisha watoto wao
wahalifu katika makundi haya kwenda mikoani ili kukwepa wasinaswe na msako huu
mkali. Hata hivyo Jeshi la Polisi lina mtandao wa kutosha kati yake na
mikoa mingine na nchi jirani hivyo litawatafuta popote walipo na kuwakamata.
Oparesheni hii ni endelevu na ya kudumu hadi kero hii ya vibaka itakavyokwisha
kabisa. Baadhi ya majina waliokamatwa ni kama ifuatavyo:-
1.
DANIEL PETER @ MALUNDE, miaka 25, mkazi wa Yombo Kigunga
2.
MWISHEHE ADAM, miaka 35, mkazi wa Mtoni mashine ya maji
3.
MOHAMED SAID, miaka 32, mkazi wa Mtoni
4.
JAKAMA ALPHONCE, miaka 23, mkazi wa Mtoni Kilakala
5.
HAMADI MDUDU, miaka 25, mkazi wa Mbagala
6.
SALUM MUSA, miaka 25, mkazi wa Kiwalani
7.
ANTHONY DANIEL, miaka 20, mkazi wa Mashine ya maji
8.
FIDELIN ANTHONY, miaka 18, mkazi wa Kigogo
9.
HAMZA MAZUMA, miaka 19, mkazi wa Kigogo
10.
MGANGA ABEID, miaka 20, mkazi wa Kigogo
11.
SAID ABEID, miaka 19, mkazi wa Kigogo
12.
SALUM NYENJE, miaka 36, mkazi wa Chamazi
13.
DOMINICK PETER miaka 22, Mkazi wa Kigogo
14.
KULWA ABEID, miaka 20, mkazi wa Mabibo
15.
MUSA IBTRAHIM, Miaka 20, mkazi wa Magomeni
16.
HUSSEIN SHABAN, miaka 22, Mkazi wa Magomeni
S. H. KOVA
KAMISHNA
WA POLISI KANDA MAALUM
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment