MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday 26 May 2014

NEWS ALERT!!!KANDA YA ZIWA KUKABILIANA NA UCHAFUZI VYANZO VYA MAJI


Ofisa  wa maji Bonde la Ziwa Victoria Jumanne Mpemba akizugumza na wandishi wa habari.
Ni mtambo unaoitwa Tera Tem, wenye kifaa maalum cha kuchunguza miamba iliyo na maji katika tabaka mbalimbali ardhini kwa kutumia mawimbi yanayotkana na umemeusumaku (Electromagnetic Conductivity Method)


Wito huo umetolewa na Afisa wa Maji Bonde la Ziwa Victoria Jumanne Mpemba wakati akiwasilisha mada ya usimamizi wa rasilimali za maji kwa pamoja katika warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari jijini Mwanza.

Alisema ili utunzaji wa vyanzo vya maji na rasilimali za maji katika bonde la Ziwa Victoria, mambo muhimu yanayotakiwa kuzingatiwa ni pamoja na kuwapo kwa usimamizi wa pamoja, ushirikishwaji wa sekta ikiwa ni pamoja na usitishaji wa shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji.


Alisema ushirikiano wenye tija unahitajika na kutaja sekta za Madini, misitu, Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Viwanda na Utalii kama maeneo yanayopaswa kushirikiana katika usimamizi endelevu wa rasilimali za maji.


"Ili kulinda Bonde la Ziwa Victoria, ni lazima kuwepo na sera ya pamoja kwa nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi zinazowiana katika utunzaji  wa rasilimali za maji katika maeneo ya nchi hizi, pia utoaji wa elimu kuhusu umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji kwa wadau na wananchi ili kuwezesha jamii inayozunguka vyanzo vya maji kutambua faida na umuhimu wake" alisema.


Mpemba ameshauri kuwako kwa mpango utakaositisha shughuli zote za kibinadamu zinazofanywa karibu na vyanzo vya maji kama Mahoteli na Viwanda kuzuia uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa vyanzo vya maji, na katika sekta ya uvuvi kuzingatia kanuni za uvuvi endelevu ili kujihakikishia ukuaji wa kiuchumi unaotokana na zao la samki ziwa Victoria.


Pia Afisa huyo amewataka wananchi na makampuni yanayotaka kutumia maji ya Ziwa Victoria au kuchimba visima kuomba vibali vya kufanya utafiri wa maji ardhini kutoka Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria kwani ndivyo inavyosema katika kunusuru ziwa hilo na vyanzo vyake kwa matumizi yasiyofaa.


“Maji ni rasilimali ya kiuchumi,ni vyema ikafahamika kuwa wananchi hawana budi kuchangia gharama kidogo ili rasilimali hii iendelee kuwepo na sheria ya rasilimali za maji ya mwaka 2009 kifungu cha 96 na 112  inamtaka kila mtumiaji maji apate kibali cha kutumia maji kwa kuomba katika ofisi ya maji,Bodi ya Bonde husika.
“Lakini  wapo wananchi wachache wenye uelewa kuhusu sheria hii wamejitokeza na kuomba vibali na kulipia ada ya matumizi ya maji ,hivyo ni vyema kila mtumiaji wa maji akaitekeleza sheria hii ili kuepuka adhabu ya kuivunja.
“Sheria  ya rasilimali za maji namba 11 ya mwaka 2009 kifungu cha 102 kifungu  kidogo cha 2 inatamka yeyote atakaye kaidi kuitekeleza adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi laki tano  au isizidi shilingi milioni moja na kama ataendelea kutolipa atatozwa faini ya shilingi milioni moja au kwenda jela miaka si chini ya mitatu”alisema

Aliongeza kuwa ili kufikia malengo ya pamoja shughuli zote za usimamizi wa matumizi ya maji ya rasilimali hiyo zinapaswa kujiendesha zenyewe, hivyo kulipa ada ya matumizi ya maji kwa wakati ni kuchangia katika uboreshaji huduma ya maji itakayo saidia kusimamia matumizi bora ya rasilimali hii.
 Na Mwanaharakati.

No comments: