William Mhando akirudishwa RUMANDE |
MKURUGENZI wa zamani wa
Shirika la Umeme nchini, (Tanesco) William Geofrey Mhando na mkewe, Eva Stephem
Mhando, na maofisa wengine watatu wa shirika hilo, France Lucas Mcharange,
Sophia Athanas Misidai na Naftali Luhwano Kisinga, wamepandishwa kizimbani
Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam kwa kosa la kuhujumu uchumi na
kuiingizia serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni 884,550,000.
Katika kesi hiyo iliyosomwa na
Wakili wa Serikali, Leonard Swai, mbele ya Hakimu Frank Mushi, wakili huyo
alisema Mhando akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco anatuhumiwa kumpa
tenda mamsap wake ya kusambaza vifaa vya stationery vyenye thamani ya shilingi
milioni 884,550,000/ kwa shirika hilo kinyume na taratibu.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment