MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 29 May 2014

WANAFUNZI IRINGA KATIKA HALI MBAYA YA UHABA WA MADAWATI HUKU WAKO KWENYE SHAMBA LA TAIFA. WANAFUNZI IRINGA KATIKA HALI MBAYA YA UHABA WA MADAWATI HUKU WAKO KWENYE SHAMBA LA TAIFA.

Na Mwanaharakati.

Kutokana na hali hiyo kuzikabili shule mbalimbali na kushusha kiwango cha elimu, moja ya shule za msingi ijulikanayo kama LUGODA LUTALI wameamua kuanzisha mpango wa kutengeneza madawati ya udongo almaarufu Adobe, ilhali wakishindwa kufaidi shamba la miti la taifa SAOHILL mkoani humo.
Wakati huo huo kila kijiji na shule wanapewa Qubick meter za shamba kwajili ya kukata na kutengeneza dawati, lakini jamii inashindwa kutekeleza hilo.

Miongoni mwa sababu zinazosababisha wasitekeleze ni pamoja na masharti ya ukataji miti na gharama za kutenegeza dawati, hivyo waandishi wamepewa changamoto ya kulifanyia kazi na kujua ni kwanini wananchi hawatengenezi madawati.

No comments: