Ni miaka 21 sasa tangu kutokea kwa ajali hiyo ambayo ilisababisha meli hiyo kutoonekana kwenye uso wa dunia.
MV Bukoba ikiwa na abiria kati ya
750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37 ilizama majini kwenye Ziwa Victoria mwambao
wa Bwiru Jijini Mwanza ambapo ilikuwa takribani kilomita 30 kufika nchi kavu.
Ripoti ya Tume ya Jaji Robert
Kisanga, iliyochunguza chanzo cha hiyo ilieleza kuwa, kati ya hao, 114
waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa
katika makaburi ya Igoma barabara ya Musoma, nje kidogo ya Jiji la Mwanza.
Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332
haikupatikana.
Kila mwaka, ifikapo Mei 21, viongozi
wa dini, wa serikali na wananchi huongozana kwenda eneo la ajali kufanya
kumbukumbu.
Hakika Mei 21 Mwaka 1996 Taifa la
Tanzania liligubikwa na Msiba Mkubwa ambapo kila mmoja kwa nanma yake aliguswa
na Msiba huo ambao uliyagharimu Maisha ya Mamia ya Wapendwa Wetu, baada ya Meli
ya MV.Bukoba Kuzama hatua chache kabla ya kutia Nanga Mkoani Mwanza ikitokea
Mkoani Kagera.
Mkoani Kagera.
Meli ya Mv.Bukoba iliyoundwa mwaka
1979 ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 850 na abiria 430 ilizama katika Maji
ya Ziwa Victoria Mkoani Mwanza yapata umbali wa kilomita zipatazo 30 kutoka
ufukweni mwa maji na kusababisha zaidi ya watu 1,000 kupoteza maisha katika
Meli hiyo ambayo tangu kuundwa kwake hadi kuzama kwake ilikuwa na umri wa miaka
17. Jambo la butwaa hapa ni Idadi ya vifo na idadi ya abiria waliookolewa
ukilinganisha na Uwezo uwezo wa Meli hiyo wa kubeba
abiria 430).
Pengine tumezoea kuita kwamba Mei 21
Watanzania tunaadhimisha kumbukumbu ya kuzama kwa Meli hiyo ambayo iliigeuza
taswira ya Mji wa Mwanza, kwani kwa waliokuwa Mwanza Mwaka huo walipigwa na
Butwaa baada ya Uwanja Mkongwe wa Nyamagana ambao mara nyingi hutumika kwa
shughuli za Kimichezo, pale ulipogeuka na ghafla na kutapakaa Maiti za wapendwa wetu, ama hakika inauma sana.
shughuli za Kimichezo, pale ulipogeuka na ghafla na kutapakaa Maiti za wapendwa wetu, ama hakika inauma sana.
Wakati leo tunakumbuka tukio hili
ambalo limeacha simanzi mioyoni mwetu, hebu tujiulize kwa pamoja; Kama ilivyo
imani ya watalaamu wa masuala ya usafiri kwamba Usafiri wa Majini ndio usafiri
salama kuliko aina nyingine ya usafiri, Je Kwa Tanzania imani hiyo ina mantiki yoyote kwamba vyombo vyetu vya usafiri wa majini ni salama?.
salama kuliko aina nyingine ya usafiri, Je Kwa Tanzania imani hiyo ina mantiki yoyote kwamba vyombo vyetu vya usafiri wa majini ni salama?.
Lakini wakati tunatafakari suala
hilo, pia tukumbuke kujiuliza sisi wenyewe bila kusubiri kusukumwa na mtu
hususani wale wenye mamlaka ya kuleta matokeo chanya katika kuboresha hali ya
usafiri majini Ikiwemo Mamlaka ya Usafiri wa nchi Kavu na Majini SUMATRA
kwamba tulijifunza jambo lolote kutokana na ajali hiyo ya Mv.Bukoba?
Na Kama kuna jambo tulijifunza, je
tumefanikiwa kulifanyia kazi ipasavyo jambo hilo? Je kuna hali yoyote ya
uwajibikaji (kwa waliopewa dhana ya kusimamia sheria) katika kuzingatia sheria
za usafiri na usafirishaji wa majini na nchi kavu? Je, tumekwisha jijengea hali
ya kuchukua hatua za uokoaji pale tunapopatwa na majanga ya majini au nchi
kavu?.
Lakini pia wapo waliohoji na bado
wanaendelea kuhoji juu ya taarifa ama ripoti ya uchunguzi wa ajari hiyo ya
Mv.Bukoba kama ulifanyiwa kazi ipasavyo? Lakini pia wakiwa bado wanaendelea
kujiuliza ni ajari ngapi za vyombo vya majini zimetokea tangu kuzama kwa meli
hiyo? Hapo nadhani nawe unazikumbuka ajali kadhaa ambazo tayari zimekwisha
kutokea na kuyagharimu maisha ya Watanzania ikiwemo ile ya mv Spice Ireland
iliyotokea Septemba 10 mwaka 2011 katika Mkondo wa Nungwi kaskazini Unguja
Zanzibar.
Lakini yote Tisa, Kumi ni stofahamu
iliyoibuka juu ya Chanzo cha ajali hiyo mbaya kuwahi kutokea hapa nchini.Wapo
waliosema ilikuwa ni Uzembe wa Wakaguzi wa na Waangalizi kwa maana ya Mamlaka
husika, Wapo waliosema ilikuwa ni Uzembe wa Nahodha na Timu yake na wapo
waliosema chombo kilikuwa kibovu.
Wapo waliodai chombo hicho kilikuwa
kimebeba Mizigo na abiria kuzidi uwezo wake na wapo waliodai kuwa abiria wenyewe
walisababisha ajali hiyo kwani walilazimisha kupanda Melini ilihali chombo
kilikuwa kimejaa huku mlolongo huo ukihitimishwa na wale waliohusisha ajali
hiyo na Imani za Kishirikina.
Mimi nasema sina nia ya kuandika
hayo yote kwa lengo la kumtafuta mchawi ila lengo langu ni kuyaweka wazi hayo
yote ili kila mmoja kwa namna anavyohusika na anavyoweza kusaidia namna ya
kufanya ili kuepukana na ajali kama hiyo ama kama ambavyo wengine husema
tusiangalie tulipoanguka bali tuangalie tulipojikwaa.
Wapo wengi waliowapoteza ndugu,
jamaa na marafiki zao na mmoja wao ambae alimpoteza mpendwa wake katika maisha
yake ni Mwanamitindo maarufu hapa nchini ambae pia anafanya shughuli zake
barani Ulaya Flavian Matata ambae yeye alimpoteza Mama yake mzazi pamoja na
binamu yake.
Pamoja na watu wengine, Matata
amekuwa na desturi ya kukumbuka tukio hilo kwa kufika Mkoani Mwanza katika eneo
la Igoma walikohifadhiwa watu waliopeza maisha katika ajali hiyo ya Mv.Bukoba
ambapo pia maadhimisho ya kuwakumbuka hufanyiia kila mwaka, huku akibainisha kuwa ilimchukua miaka mingi hadi kuamini kuwa ni kweli hayuko na mama yake mzazi, kwa kusema kuwa ni miaka michache iliyopita ndiyo ameweza kuamini kama ni kweli hayuko na mama yake tena.
ambapo pia maadhimisho ya kuwakumbuka hufanyiia kila mwaka, huku akibainisha kuwa ilimchukua miaka mingi hadi kuamini kuwa ni kweli hayuko na mama yake mzazi, kwa kusema kuwa ni miaka michache iliyopita ndiyo ameweza kuamini kama ni kweli hayuko na mama yake tena.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment