Mkoa wa Kagera unaendelea na utambuzi wa
maeneo yenye uhitaji ya miradi mikubwa ya maji, na tayari umetenga shilingi
bilioni 6 na milioni 36 kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi 22.
Fedha hizo zimetengwa katika mwaka wa fedha
2017/18, utakaoanza utekelezaji wake Julai mwaka huu.
Akizugimza na mwandishi wa mtadao huu,
mhandisi wa maji mkoani Kagera Avitus Exavery, amesema kuwa miradi hiyo
itatekelezwa katika halmashauri zote nane mkoani humo, na kati ya miradi
hiyo mradi wa Kyerwa umepewa kipaumbele na unatarajiwa kutumia shilingi
milioni 800, kwa ajili ya usanifu na utahudumia vijiji 57 vyenye wakazi laki
moja na elfu 26.
Amehitaja baadhi ya miradi mingine itakayotekelezwa, kuwa ni katika vijiji vya Nyakabulala, Kyamalange,
Kashenge, Omurunazi, Kiteme na Kigazi, vya halmashauri ya Muleba na Bukoba.
Mhandisi Exavery amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa halmashauri husika, ili
kuweza kuibua miradi ya maji katika maeneo yenye uhitaji zaidi, pamoja na
kuhakikisha wanatunza miradi hiyo, ili kuepukana na uharibifu ambao umekuwa ukijitokeza.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment