MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 20 May 2017

UGONJWA WA EBOLA WA AMSHA MAKALI YA SERIKALI KAGERA.



Serikali mkoani Kagera, imeanza kuchukua taadhari za ukaguzi wawageni wanaoingia nchini kupitia mipaka ya mkoa huo, kujua kama wana maambukizi ya ugonjwa wa ebola uliripotiwa nchini DRC.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wauguzi kimkoa iliyofanyika katika hospitali teule ya Rubya, mganga mkuu wa mkoa wa Kagera Dr. Thomas Rutachunzibwa,  amesema kuwa ugonjwa huo haujaingia nchini lakini wameanza kuchukua hatua za kuudhibiti.

Amesema kuwa pamoja na ukaguzi kufanyika mipakani, tayari waganga wakuu wa wilaya wameagizwa kuhakikisha wanatoa elimu juu ya ugonjwa huo kwa wananchi, ili waweze kuutambua na kuchukua taadhari.

Akizungumza na waandishi wa habari wiki hii, katibu wa wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto  Dk. Mpoki Ulisubisya, aliwataka wananchi walioko katika mikoa ya Mwanza, Kagera, Kigoma, Rukwa, Katavi na Songwe, kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya juu ya ugonjwa wa ebola.

Dr. Rutachunzibwa amewataka wauguzi  elfu moja na 328 waliopo mkoani Kagera, kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na kiapo cha kazi yao, ili kiwe mwongozo katika utendaji wa kazi zao.

Katibu wa chama cha wauguzi mkoani Kagera –TANNA, Bi Georgina Sebastian, wakati akisoma risala kwa mgeni Rasmi, amesema kuwa pamoja na mafanikio kwenye  sekta ya afya mkoani humo, bado kuna changamoto za ukosefu wa maeneo ya kutolea huduma kuwa na upungufu wa vitendea kazi kama dawa na vifaa tiba.
 

Na Mwanaharakati.

No comments: