Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda, amesisitiza umuhimu wa
elimu ya masafa ya chuo kikuu huria, kuwa ni muhimu kujiendeleza ukiwa mahala
pa kazi.
Mh. Pinda amesema hayo wakati wa mahafali ya 29 ya chuo
kikuu huria cha Tanzania, yaliyofanyika kwa mara ya tisa katika viwanja vya
makao makuu ya chuo hicho Bungo Kibaha mkoani Pwani, kwa wahitimu 4,265 kutunukiwa
shahada ya udhamivu, stashaada na ngazi ya cheti.
Amesema kuwa elimu ya masafa ilibezwa na kusababisha kiwango
cha elimu nchini kutokupanda, akimwomba mkuu wa chuo hicho Dr Asha Rose Migiro,
kudumisha mahusiano katika nchi za nje ili kupeana uzoefu jinsi ya ukuzaji wa
elimu bora.
Udahiri wa wanafunzi wapya umeongezeka kutoka elfu 10 wa
awali hadi laki moja kwa muhula ambapo
uongozi wa chuo hicho kwa sasa unafanya utaratibu wa kuendelea kutumia Tehama kufundishia
ili kupunguza gharama za uendeshaji na kuweka majengo katika mikoa ambayo bado,
na kufanya ukarabati katika baadhi ya maeneo.
Tangu chuo hicho kuanza hapa Tanzania, kimekwisha
kuhitimisha wanafunzi 26,241, ambapo kimeweka vituo nchi za Rwanda, Namibia,
Malawi na Kenya, na katika mahafali ya 29 mwaka huu, Bi Anne Kilango Malecela,
mkuu wa mkoa Kagera John Mongela na aliyekuwa mkuu wa wilaya Kinondoni Jerry
Slaa ni miongoni mwa wahitimu waliotunukiwa shaada.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment