Takriban Washiriki 450 wakiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri 28 za Tanzania wanahudhuria mkutano huo, ambao unafanyika katika viwanja vya GYMKHANA, katika manispaa ya BUKOBA.
Picha juu ni katika kuimba nyimbo za mataifa shiriki.Washiriki wa Mkutano huo, jana, walishiriki katika shughuli za hifadhi mazingira na upandaji miti katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya BUKOBA.
Hatua hiyo ni kuunga mkono jitihada za Mkuu wa mkoa wa KAGERA, kanali mstaafu FABIAN MASAWE.
Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, bwana AGGREY MWANRI, ambaye pia amehudhuria mkutano huo, anatarajia kuufunga mkutano huo.
Kasibante fm Redio kama kawaida yetu tukarusha matangazo ya moja kwa moja kutoka viwanjani hapo.
No comments:
Post a Comment