Mwenyekiti wa Umoja huo hapa nchini, Dk ANATOLI AMANI amesema kuwa Mkutano huo wa LVRLAC, utaenda sambamba na viongozi hao kufanya usafi
katika maeneo mbalimbali ya manispaa ya Bukoba.
Hatua hiyo ni
kuunga mkono jitihada za Mkuu wa mkoa wa KAGERA, kanali mstaafu FABIAN MASAWE.
Wakurugenzi wa Halmashauri, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri
28 za Tanzania ambao wanahudhuria
mkutano huo, jana, walishiriki
katika semina ya kuwajengea uwezo namna ya kubuni miradi ya maendeleo katika Halmashauri
zao ili kuongeza mapato.
Katika semina hiyo, baadhi ya Halmashauri zimependekeza miradi
kadhaa ya maendeleo ambayo zitaitafutia wafadhili.
Halmashauri za
mkoa wa KAGERA kwa pamoja zimependekeza
ujenzi wa maegesho mapya ya magari, ujenzi wa viwanja bora vya michezo, pamoja na kuimarisha msitu wa BURIGI, kuwa moja ya kivutio cha utalii mkoani KAGERA.
Akifunga semina hiyo ya siku moja, Mkuu wa wilaya ya
BUKOBA, bi ZIPORRAH PANGANI amewataka
viongozi hao kujenga desturi ya kuwashirikisha wananchi katika kupanga na
wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kama ilivyo ada kunapokuwa upokeaji wa geni lazima usafi uzingatiwe, hii ni shimo la taka ambalo linakaa na uchafu muda mrefu lakini sasa naona itifaki imezingatiwa.
No comments:
Post a Comment