Afisa uhusiano manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu, amesema
kuwa katika mwaka wa fedha 2010/11,
walipanga kukusanya bilioni 2.8 lakini wakakusanya bilioni 2.1, mwaka 2012/13
walipanga kukusanya bilioni 4, lakini walikusanya bilioni 1.8, na hivyo
kusababisha hasara serikalini, ambapo katika mwaka wa fedha 2015/16 manispaa inatarajiwa
kukusanya bilioni 11.5.
Amesema kuwa viwango vya kodi ya majengo vimetajwa kweenye kifungu
namba tatu, kifungu kidogo cha kwanza
cha sheria ya ardhi nyumba na makaazi, ambapo imefafanuliwa kuwa nyumba ya
biashara na viwanda inatozwa 0.2% ya thamani ya jengo zima , nyumba ya makazi inatozwa 0.15% kwa mwaka, huku
akitaja sababu mbalimbali za kushindwa kutimiza malengo ya ukusanyaji kodi.
Meneja wa kodi ya majengo halmashauri ya manispaa ya Ilala Bw. Kajuna,
imejipanga kuanza utaratibu wa kuchukua taarifa upya kwa usahihi, kurahisha huduma
za malipo kupitia mitandao ya kijamii, na kuanza kutuma ujumbe kwa kila mlipa
kodi kupitia simu ya mkononi, ili kukumbushia deni na jinsi ya kulipa.
Novemba 2015, serikali ilitangaza kuanza kutumika kwa mfumo
wa kielektroniki yaani ulipaji kwa njia ya mtandao Tehama, kukusanya kodi za majengo na huduma
mbalimbali, huku ikianzisha dawati la usaidizi kwenye halmashauri zenye shida
ya mtandao, ili kuondoa ulipaji kodi kwa muhasibu, baada ya kubaini upotevu wa
fedha zinazolipwa.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment