Mbunge wa Kinondoni, Maulidi Mtulia akihojiwa na waandishi baada ya kutoka katika mahakama Kuu ya ardhi |
Umati
wa wananchi wa Mabondeni ikiwemo bonde la Msimbazi, Magomeni Mkwajuni,
Hananasifu, Magomeni Sunna, Kigogo na maeneo mengine wa Jimbo la
Kinondoni wamefurika kwa wingi mapema kuanzia asubuhi ya leo katika
Mahakama Kuu ya Ardhi iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam
kusikiliza kesi ya msingi ya kupinga kubomolewa nyumba zao
iliyofunguliwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Mh. Maulidi Mtulia (CUF).
Mtulia
amefungua kesi hiyo kupinga kubomolewa kwa wakazi hao bila kuwa na njia
mbadala ikiwemo kupatiwa makazi mengine kwa wananchi wake yenye usalama
zaidi.
Hata
hivyoi Modewjiblog iliyokuwa katika eneo la tukio tokea asubuhi,
ilishuhudia umati mkubwa wa wananchi wakifurika katika viunga vya
Mahakama hiyo kiasi cha kufanya shughulo zingine za mahakama hiyo
kusimama.
Baada
ya masaa matatu, Jaji wa Mahakama hiyo Kuu ya Ardhi, Mh. Panterine
Kente aliweza kusimamia kesi hiyo huku baadhi ya wananchi wakiwakilishwa
na wajumbe zaidi ya saba, pamoja na wanasheria wa Mbunge huyo, ambapo
maamuzi yalidumu kwa muda wa saa zaidi ya saa moja, na baadae Mawakili
wa upande wa Mbunge wa Kinondoni, akiwemo Abubakari Salim aliweza
kuutangazia wananchi hao pamoja na wanahabari kuwa, baada ya kupitia
vielelezo vyote, kesi hiyo itatolewa hukumu kesho siku ya Jumanne,
Januari 5.2016.
“Kwa
shahuri lililopo sasa linatarajiwa kutolewa jibu kesho Januari 5, Saa
tano asubuhi ndio tutapata jibu kamili, kwa sasa tunarudi na tutakutana
hapa hapa Mahakamani.” alieleza Wakili huyo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment