Bahrain imetangaza kwamba imevunja
uhusiao wa kibalozi na Iran, saa chache baada ya Saudi Arabia kuchukua hatua
sawa.
Saudi Arabia iliwapa wanabalozi wa
Iran siku mbili kuondoka nchini Saudi Arabia kufuatia
mvutano uliotokana na kuuawa kwa mhubiri maarufu wa Kishia.
Bahrain hutawaliwa na Mfalme Msuni
lakini raia wengi ni wa dhehebu la Shia.
Ufalme huo pia umewapa wanabalozi wa
Iran saa 48 wawe wameondoka nchini humo.
Sudan nayo imemfukuza balozi wa Iran
kutoka Khartoum huku muungano wa Jumuiya ya Milki za Kiarabu UAE nayo
ikipunguza idadi ya maafisa wa ubalozi. Waislamu wengi nchini Sudan ni Wasuni.
Mhubiri huyo Sheikh Nimr al-Nimr
aliuawa pamoja na watu wengine 46 baada ya kupatikana na makosa yanayohusiana
na ugaidi.
Washia walishutumu hatua hiyo na
maandamano yalishuhudia maeneo yenye Washia wengi.
Mjini Tehran, waandamanaji
waliteketeza majengo ya ubalozi wa Saudi Arabia.
Saudi Arabia na Iran ndiyo mataifa
makuu ya Kisuni na Kishia mtawalia Mashariki ya Kati, na yamekuwa yakiunga
mkono pande pinzani katika mizozo inayoendelea Syria na Yemen.
Kuna wasiwasi huenda machafuko
yakatokea kanda hiyo.
Jumatatu, misikiti miwili ya Wasuni
ilishambuliwa na imam mmoja akauawa.
Saudi Arabia ilitangaza
kwamba imekatiza uhusiano wake na Iran baada ya maandamano yaliyotokea ubalozi
wake mjini Iran. Ilisema pia kwamba imemwagiza balozi wake arejee nyumbani.
Wizara ya mambo ya nje ya
Iran imesema Saudi Arabia inaendeleza sera ya kuzidisha chuki na makambiliano
katika kanda hiyo.
Msemaji wa wizara hiyo
Hossein Jaber Ansari alisema Jumatatu kwamba Saudi Arabia inajaribu kusuluhisha
matatizo yake ya kinyumbani kwa “kuyatoa nje kwa mataifa mengine”.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment