.Ni ukosefu wa mwongozo
Serikali kupitia wizara ya fedha, inaandaa mwongozo mpya chini
ya sheria ya fedha namba 38, ili kuondoa ubadhilifu unaojitokeza nchini.
Mkaguzi mkuu wa ndani wa serikali Bw. Mohamed Mtonga,
amesema kuwa sheria ya fedha inaelekeza kuandaliwa kwa mwongozo huo,ambao
utahakikisha majukumu ya idara yanatekelezeka kwa kuwezesha wakaguzi wa ndani
wanatimiza majukumu yao kwa kina, na kuhakikisha masuala ya utawala bora
yanatekelezwa ipasavyo.
Hatahivyo bwana Mtonga amesema kuwa, idara ya ukaguzi wa
ndani ina taarifa nyingi na nzito kuliko za CAG, ila zinahishia kwenye utawala
kutokana na mfumo uliopo, kwa kusisitiza kuwa kuna uwezekano halmashauri kupata hati safi baada ya utafiti wa ndani
lakini ikawa tofauti baada ya kufanyiwa ukaguzi na mkaguzi mkuu wa serikali CAG.
Idara ya mkaguzi mkuu wa ndani wa serikali, inafanyakazi
katika wizara ya fedha ikiwa na vitengo vya uhakika wa ubora, usimamizi
viashiria hatarishi, ukaguzi wa bajeti na mishaara, ukaguzi wa kiufundi na
kitengo cha ukaguzi wa serikali za mitaa, ambavyo kwa pamoja vinanafasi ya
kufanya ukaguzi maalumu wa kiuchunguzi, kulingana na mahitaji ya kitengo
husika.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment