Sukari ikiwa katika bei ya shilingi 2500 kwa kilo katika maduka bado upatikanaji wake umeleta shida na hapa katika kituo cha uuzaji sukari cha KAGERA SUGAR njini bukoba na hawa ni wafanyabiashara.
Katika kipindi cha karibuni imetangazwa operesheni ya kukamata wanaovusga sukari hiyo kwenda nchi za nje kutokana na kuadimika kwa bidhaa hiyo hapa nchini jambao ambalo linaonekana kuleta mafanikio kwa kiasi kikubwa.
Wiki hii mkoani kagera askari walifanikiwa kukamata kiasi flani cha sukari na kukirudisha mikononi mwa serikali lakini kinachosikitisha ni kuwa sukari hiyo inauzwa kwa bei ya shilingi laki moja tofauti kabisa na aagizo la waziri mkuu kwamba ikikamatwa iuzwe kwa bei ambayo wenye maduka watauza kwa kilo shilingi 1700.
No comments:
Post a Comment