Ni katika barabara ya Babati mkoani arusha ambapo basi la kampuni ya ZUBER likiwa linatokea Arusha kulekea mwanza lilionekana kuwa na mapungufu katika safari hiyo jambo lililopelekea kusimamishwa mara kwa mara askari wa usalama barabarani.
Baada ya kusimamishwa askari hawa wamekuwa wakimwita pembeni kondakta wa gari hiyo na katika kile kinachooneka katika video hii ni pale askari wakipokea kitu kunachosadikika kuwa ni hela.
Abiria waliokuwa katika gari hiyo ususani wale waliozoea kusafiria magari ya kampuni hiyo wamesema magari yanayoonekana kuwa na mapungufu usimamishwa kila wanapokutana na askari kwa sababu askari hao upeana taarifa ni jinsi gani watakavyozungumza nao kuhusu chochote.
No comments:
Post a Comment