Ni mchanganyiko wa magari ya binafsi na ya biashara lakini yote yakisubiri abiria katika stendi ya Bihalamuro.
Katika stendi ya mabasi wilayani bihalamuro mkoani kagera kumekuwa kukithiri kwa matumizi ya magari binafsi kubeba abiria jambo ambalo ni kosa katika taratibu za usalama barabarani.
Madereva na makondakta wanaotumia stendi hiyo wamesema kuwa kila siku magari yao ukaguliwa askari wa usalama barabarani na jambo hilo analiona lakini kutokana na kuwa inasemekana wenye magari hayo wanafahamiana na mengine ni baadhi ya askari hao jambo hilo linaendelea kuwepo.
Pia wamesema inavunja moyo wale ambao wanafuata sheria za biashara hiyo na tofauti na hiyo magari hayo kiuka taratibu kwa kujaza abiria kupita kiasi lakini askari uangali na kuona kinachoendelea.
Stendi ya Bihalamuro ipo katika wilaya hiyo na inahusisha magari yaendayo sehemu mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment