MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday 29 April 2014

MALI ZA MZEE GURUMO ZAGOMBANIWA


 Kwa mujibu wa chanzo ambacho ni ndugu wa karibu wa familia hiyo, siku moja baada ya msiba, mtoto huyo alitangaza kuwa gari hilo ni lake na akaanza kutafuta madalali wa kuliuza gari hilo lakini akakwamishwa na kukosekana kwa kadi ya gari.

“Yaani hawa watoto wa marehemu sijui wana nini jamani, hata arobaini ya baba yao bado wameanza kushikana mashati, hii ni hatari sana. Huyo mmoja ndiyo anajitapa kabisa kuwa gari ni la kwake na ameshaanza kutafuta mteja,” kilisema chanzo chetu kwa masharti ya kutotajwa gazetini.
 Mtoto wa marehemu, Mariam Gurumo ambaye alipoulizwa kuhusu ishu hiyo, alisema: “Aliyekupa hizo taarifa ni muongo, hakuna ishu kama hiyo. Kwanza bado tunaomboleza kifo cha baba yetu. Sasa tuuze gari na nyumba ili iweje? Siyo kweli.

“Ni kweli kuna kesi ya nyumba ipo mahakamani lakini siyo nyumba hiyo unayoisema. Unajua sisi watoto wa Gurumo tunataka kudhulumiwa nyumba iliyoachwa na marehemu mama yetu iliyopo Ilala. 

“Unajua huyu mjane wa marehemu, hakubahatika kupata mtoto, sisi mama yetu ni marehemu na tulizaliwa wanne, mimi (Mariam), Mwalimu, Mwazani na Omary.

“Abdallah yeye ana mama mwingine lakini ni ndugu yetu wa damu. Kabla mama hajafa, Gurumo alimjengea nyumba Ilala.
“Sasa mama yetu alipokufa, mdogo wake (jina tunalihifadhi) akawa anataka kuiuza, hivi jana tu (Ijumaa) tumetoka mahakamani. Tumefungua kesi pale yenye jalada namba RB/IL/112/2013 kuzuia nyumba kuuzwa. Tunashukuru mahakama imeingilia kati vinginevyo tungedhulumiwa.

Naomba watu wasichanganye, nyumba yenye matatizo ni ya Ilala. Kuhusu gari, kwa sasa bado hatujaamua chochote mpaka arobaini ipite,” alisema Mariam.
Mariam Gurumo



“Ni kweli nyumba inauzwa. Hilo lilikuwa ni agizo la mume wangu kabla hajafariki, aliniambia ni bora aiuze kabla hajafa kwani anawajua wanaye watanisumbua sana pindi akifa.
“Tulianza kutafuta wateja miezi minne kabla Gurumo hajafa, bahati mbaya ametangulia kabla hatujakamilisha hiyo kazi. Yeye alikuwa na lengo zuri la kutaka atugawie kila mmoja chake ili akifa yasitokee haya yanayotaka kutokea.

“Unajua hii nyumba tumejenga na mume wangu, mimi nilikuwa mfanyabiashara na tulisaidiana kabla hata hawa watoto hawajazaliwa lakini nashangaa wanataka kunigeuka eti mimi sihusiki.”
“Naomba serikali iingilie kati kwenye hili suala, nyumba wala gari viziuzwe kwanza. Jamani hata eda sijamaliza mambo yameanza kuwa hivi.

Hao watoto wenyewe tangu tumzike baba yao hawajakanyaga hata hapa nyumbani kunijulia hali, sijui wanafikiria nini kuhusu mimi, naomba mnisaidie nimalize eda salama na mali zikiuzwa, basi na mimi nipewe staahili yangu,” alisema mjane huyo kwa huzuni.

Na Mwanaharakati.

No comments: