Kamanda wa polis Singinda George Kamwela amethibitisha kuwa ni watu 19 atatoa taarifa punde kwa majina halis hAyajapatikana lakini majeruhi ni 8 mmoja akiwa na hali mbaya.
|
SUMRY
WATU 19
akiwemo askari wa kikosi cha usalama barabarani wamepoteza maisha baada ya
kugongwa na basi la kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar
katika kijiji cha Ikungi mkoani Singida usiku huu.
Ajali hiyo
imetokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori lililomgonga mwendesha
baiskeli aliyepoteza maisha papo hapo na wakati wananchi wakiwa wamekusanyika
eneo hilo la ajali huku trafiki akiendelea kupima ajali hiyo, lilitokea basi la
kampuni ya Sumry na kuwagonga watu hao pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya
watu 14 kupoteza maisha eneo hilo.
Basi hilo
lililokuwa likitokea Kigoma kwenda Dar halikuweza kusimama eneo hilo mpaka
dereva wake alipokwenda kujisalimisha kituo cha polisi Ikungi, Singida.
Miili 14 ya waliopoteza maisha
katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja
na majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini hapo.
|
No comments:
Post a Comment