Wanafunzi
wa Kidato cha Tano na sita, katika Shule ya Sekondari ya Lukole, iliyopo
wilayani Ngara mkoani Kagera wanalazimika kutembea umbali wa kilomita
saba kufuata huduma ya maji, kutokana na kuharibika kwa mashine ya kusukuma
maji.
Akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi hao, wakati wa mahafali ya nne ya kidato cha sita, Ishengoma Edibily amesema kuwa kutokana na kuharibika kwa mashine hiyo, inayosimamiwa na idara ya maji, wanalazimika kukatisha baadhi ya masomo.
Ishengoma
amesema kuwa, hali hiyo inawaathiri Kitaalaum kutokana na kutumia muda wingi wa
kujifunza kutafuta maji.
Amesema
kuwa mbali na shule hiyo kukabiliwa na ukosefu wa huduma ya maji, pia
inakabiliwa na ukosefu nishati ya umeme na upungufu wa vitabu kwa ajili ya kufundishia
na kujifunzia masomo.
Akizungumza
katika mahafali hayo, Mkuu wa wilaya ya Ngara Bwana Costantine Kanyasu amesema
kuwa, wananchi wa eneo la K9 wataondokana na tatizo la ukosefu wa maji baada ya
kufungwa mashine na nishati ya umeme.
Bwana
Kanyasu amesema kuwa, halmashauri ya wilaya ya Ngara tayari imepokea zaidi ya
Shilingi milioni 80 kutoka Ofisi ya Rais, na kuwa mashine itakayofungwa katika
chanzo cha maji cha K9 itasaidia kuwapatia maji wakazi wa eneo hilo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment