MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 2 May 2014

MAKAMU WA RAIS AMEONGOZA UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE BUKOBA

 Mwenge wa uhuru ulizinduliwa katika uwanja huu mwaka 2004, kwahiyo kuzinduliwa hapo leo kumefanyika baada ya miaka 10 iliyopita, ambapo utazindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 15.6.
Mh Bilal akiuwekea moto mwenge huo
Mwenge huo unaoongozwa na Rachael Stephen Sanda kutoka Tabora, katika manispaa utazindua miradi 10  na unatarajiwa kulala kata Kashai, ili kuelekea Muleba, Bukoba v, MIsenyi na hatimaye Kyerwa na Karagwe, ili kuhitimisha na Ngara tarehe 14 utakapokabidhiwa kwa mkoa wa Kigoma.
Makamu wa Rais baada ya kuwasha mwenge sasa anakabidhi kwa mkuu wa mkoa Mh Fabian Massawe.

Mkuu wa mkoa Massawe akiukabidhi kwa kiongozi wa mbio za mwenge Bi Rachel Kasanda.

Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia kwa karibu hotuba ya makamu wa rais.

Katika uzinduzi huo, makamu wa rais ametumia ujumbe wa mbio hizo mwaka huu, kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi, katika kuipitisha katiba mpya itakaporejeshwa kwao baada ya kukamilika kwa uchambuzi ya rasimu huko katika Bunge maalumu.

Kauli mbiu ya mwaka huu "JITOKEZE KUPIGA KURA YA MAONI TUPATE KATIBA MPYA".
Na Mwanaharakati.

No comments: