![]() |
Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwasilisha taarifa ya sura ya Bajeti
kuu ya Serikali kwa wabunge leo (jana) jijini Dar es salaam inayotarajia
kuanza kutumika kwa mwaka wa fedha unaoanza Julai 2014/2015.
|
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa
Fedha Saada Mkuya Salum alipokuwa akiwasilisha taarifa ya sura ya Bajeti kuu ya
Serikali inayotarajia kuanza kutumika mwaka wa fedha unaoanza Julai 2014/2015
leo (jana) jijini Dar es salaam.
Waziri Saada alisema kuwa mfumo wa bajeti
kwa mwaka wa fedha unaoanza unazingatia sera za bajeti kwa mwaka 2014/2015
ambazo zitazingatia vipaumbele vya mpango wa Maendeleo wa Taifa na
malengo ya utekelezaji wa mkakati wa matokeo makubwa sasa (BRN).
Kwa upande wa matumizi ya kawaida
Serikali inatrajia kutumia jumla ya sh.trilioni 14, 208. 21 ambayo inajumuisha
mfuko mkuu wa serikali, mishahara ya watumishi wa Serikali, wizara, mikoa,
halmashauri, taasisi na wakala za Serikali.
Aidha, kwa matumizi mengine yatakuwa
ni kwa ajili ya maendeleo kwa mwaka wa fedha unaotarrajiwa kuanza Julai mwaka
huu ambapo kiasi cha 5, 445.10 ambazo ni sawa na asilimia 27.7 zimepangwa
kutumika kwa kuhusisha fedha za ndani na za nje ya nchi.
Waziri Saada akiwasilisha taarifa
yake kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wabunge hao
waliipokea Taarifa ya Serikali kuhusu Makadirio ya Bajeti katika Ukumbi wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam ambayo inatarajiwa kuongeza
wigo wa wabunge kuijadili bajeti hiyo kabla ya kusomwa bungeni mjini Dodoma.
Shabaha ya bajeti ya mwaka ujao wa
fedha ni kuhakikisha pato la taifa litakuwa kwa asilimia 7.2 mwaka 2014,
asilimia 7.4 mwaka 2015, asilimia 7.7 mwaka 2016 na kuendelea kuongezeka hadi
kufikia asilimias 8.0 ifikapo mwaka 2017.
Misingi ya bajeti ya Serikali kwa
kipindi cha mwaka 2014/2015 ni pamoja na kuendelea kuwepo na kuimarishwa amani,
usalama, utulivu na utengamano misingi ambayo itasaidia kupatikana kwa katiba
mpya kwa wakati kama ilivyopangwa.
Kwa upande wake Waziri wa nchi,
Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu Stephen Wasira akiwasilisha rasimu ya
mpango wa maendeleo wa taifa katika bunge likikaa kama kamati alisema kuwa
maeneo ya vipaumbele yanalenga miradi ya kitaifa ya kimkakati
inayolenga kutanzua vikwazo vikuu vya kiuchumi inajumuisha miundombinu ya
uasfirishaji kama reli, barabara, bandari, na usafiri wa anga.
Vipaumbele vingine ni nishati,
huduma ya maji mijini na vijijini, kilimo, viwanda, maendeleo ya rasilimali
watu na huduma za kiuchumi kama fedha, biashsra na utalii.
Naye Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amewaasa wabunge wote
washiriki kikamilifu katika kamati pamoja na serikali ili ipatikane bajeti
yenye tija kwa taifa na wabunge waikamilishe kizalendo kwa kujali nchi yao.
Kikao cha Bunge la bajeti kinatanguliwa na kamati
mbalimbali zitakutana ambapo vikao vilianza Aprili 27, 2014 kwa wajumbe
kuwasili jijini Dar es salaam na kuhitimishwa Mei 4, 2014 na wabunge kuanza
safari kwenda Dodoma tayari kwa kuanza kikao chake kama ilivyopangwa.
Kamati ya bunge
ya Kilimo, Mifugo na Maji, kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili
na Mazingira wakati wa Bunge la bajeti, kamati ya kudumu ya Bunge ya
Miundombinu, kamati ya Nishati na Madini, kamati ya Bunge ya hesabu za
Serikali (PAC) kujadili hesabu zilizokaguliwa za Serikali kuu na mashirika ya
umma, kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Na nyingine ni kamati ya kudumu ya
Bunge ya Huduma za Jamii, kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa, kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na
Utawala, kamati ya kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na
Biashara, kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya UKIMWI, kamati ya
LAAC Dar es salaam na kamati ya kudumu ya bunge ya maendeleo ya jamii.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment