Ni daraja la Kanoni manispaa ya
Bukoba, lililogharimu zaidi ya milioni 300,
ambapo lilizinduliwa mapema mwezi januari mwaka huu, siku mbili kabla ya CAG
kusoma ripoti kuhusu utekelezaji wa miradi katika manispaa ya Bukoba.
 |
| Hii ndiyo hatua ya ukarabati wa sasa ambapo linawekwa zege baada ya kukwangua lami iliyokuwapo awali. |
 |
| Ni baadhi ya wasafiri na vyombo vyao wakisubiri kupishana baada ya upande mmoja wa daraja hilo kufungwa baada ya kumwaga zege. |
 |
| Hii ni picha inayoonesha daraja hilo siku chache baada ya kuzinduliwa na mkuu wa mkoa kanali mstaafu Fabian Massawe mwishoni mwaka jana. |
 |
| Picha ikionesha ukarabati uliofanywa wakati wa ujio wa Mh Rais wakati wa mazishi wa Profesa Kazaura. |
Meneja wa TANROADS mkoa Bw John Kalupare, alipozungumza na kandataziwa, alisema kuwa kuna muda wa miezi sita ambao daraja hilo linatakiwa kukabidhiwa kwa Tanroads, lakini mkuu wa mkoa alipendekeza daraja hilo lifunguliwe kwa ajili ya kutumika na akalizundua, hivyo wakandarasi watendelea kulikarabati mpaka watakapolikabidhi, baada ya miezi hiyo 6 kutimia ambapo hatahivyo zimebaki siku chache.
Draja la Kanoni, lilizinduliwa mwezi Desemba 2013, muda mfupi kabla ya CAG kutoa ripoti yake kuhusu ubadhilifu wa fedha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika manispaa ya Bukoba, ambapo wakati huo lilikuwa limekengwa kwa lami juu, ambayo hatahivyo baada ya kuanza kutumika lilianza kuvimba na kuchimbika mashimo hali iliyowapa wasiwasi wananchi na kuanza kulalamikia serikali kuwa imetafuta fedha za wananchi milio zaidi ya 300.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment