![]() |
| Picha ikionyesha aliyekuwa mwenyekiti vijana Chadema kata ya Orturumenti Thomasi Kivuyo akichukua kadi. |
|
Katibu wa vijana wilaya ya Arumeru akiwa
Boniface Mungaya akionyesha baadhi ya kadi zilizorudishwa na wanachama wa
Chadema.
|
Tukio hilo lilitokea hivi karibunii wakati wa mkutano wa hadhara wa Chama Cha Mapinduzi uliofanyika katika kijiji cha Elikiushing kilichopo wilayani Arumerumkoani Arusha
Akiongea wakati wa kurudisha kadi ya Chadema na kukabidhiwa kadi ya CCM mwenyekiti wa vijana wa Chadema Thomasi Molel alisema kuwa ameamua kuchukuwa hatua hiyo mara baada ya kuoana kuwa tangu awe katika Chama Cha Chadema ajapata faida yeyote wala ajaona kitu ambacho wananchi wanafaidika kupitia chama hicho.
Alisema kuwa yeye ni mwanasiasa mzoefu kwani alianza kuingia katika siasa tangu mwaka 1995 na anajua siasa vilivyo hivyo ameamua kuondoka katika chama hicho kwani Chadema ni chama ambacho akina democrasia ya kweli ambayo inatakiwa iwenacho kama chama.
Alisema kuwa viongozi wengi wa Chadema wamekuwa wanatoa ahadi za uongo kwa wananchi na mbali na hicho pia chama hicho kimekuwa na wasemaji wengi kwani kila kiongozi amekuwa anasema anachotaka badala ya kuwa na msemaji mmoja ambaye ndie atake weza kukisemea chama .
Aidha alibainisha kuwa katika kata yao tangu upinzani wameingia madarakani hamna kitu ambacho wamewafanyia wananchi badala yake wamekuwa wakiwachangisha wananchi hela nyingi bila kufanya maendeleo yeyote akitolea mfano mchongo wa shilingi elfu mbili ambao ulichangishwa kwa kila mwananchi wa kike na kiume ikisemekana hela hiyo ingeweza kujengea shule lakini hadi leo hela ile aijafanya chochote na aijulikani ilipopelekwa.
Aliongeza kuwa kingine ni kile kitendo cha kutosomewa mapato na matumizi ya kata yao tofauti na kipindi ambacho CCM ilikuwa madarakani hivyo.
Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Arumeru Godfrey Sabuni alisema kuwa wao kama CCM wanawapokea wananchama hao na pia wamesikia baadhi ya matatizo yao likiwemo la kutosomewa bajeti ya mapato na matumizi kwa kipindi kirefu na aliwaaidi kufuatilia swala hili kwa kwenda katika ofisi ya mkurugenzi kufuatilia swala hili.
Aliwasihi wananchi kutofanya makosa katika kipindi hichi kunakoelekea uchaguzi mdogo wa viongozi wa vijiji na vitongoji kwani wakifanya kosa kwa kuchagua viongozi wabovu wataendelea kuteseka na kata yao haitapata viongozi wazuri.
Picha ikionyesha baadhi ya wanachama waliojiunga na
CCM wakila kiapo katikati ni aliyekuwa mwenyekiti vijana Chadema kata ya
Orturumenti Thomasi Kivuyo.
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment