Shambulio limetokea katika jimbo la
Yobe nchini Nigeria wakati watu wakitazama mechi za kombe la dunia.
Jimbo hilo limewekwa katika hali ya
hatari huku maafisa wa usalama wakijaribu kukabiliana na mashambulio
yanayofanywa na wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Wakaazi wanasema walisikia sauti ya mlipuko
mkubwa nje ya eneo la kutazama sinema mjini Damaturu ambapo mashabiki wa soka
walikua wamejumuika kutazama mechi za kombe la dunia.
Walioshuhudia wanasema mshambuliaji
wa kujitolea mhanga aliyekuwa amebebwa kwa baiskeli alijilipua karibu na
mgahawa katika jimbo la Yobe wakati mechi kati ya Brazil na Mexico ikiendelea.
Mfanyikazi mmoja wa hospitali amewaambia waandishi habari kuwa waliopelekwa hapo wana majeraha mabaya huku baadhi yao wakipoteza miguu na mikono.
Wiki iliyopita maafisa wa utawala katika jimbo la Adamawa ambalo liko katika eneo hilo la Kaskazini mwa Nigeria walipiga marufuku watu kujumuika katika maeneo ya umma kutazama mechi za kombe la dunia kutokana na hofu ya Usalama.
Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya shambulio kutokea katika eneo la burudani na kusababisha mauaji ya watu kadhaa.
Hali ya hatari
Majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa yako katika hali ya tahadhari kuanzia mwezi Mwezi 2013 kufuatia mashambulizi ya kila mara ya wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram..Takriban watu 2,000 wamepoteza maisha yao yangu visa vya uasi kuanza kutekelezwa mwaka wa 2009.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment