. Wasema vyama vitumie lugha sahihi,
. Wadau wavinyooshea vyombo vya habari,
Ni katika kongamano lililoandaliwa na chama cha waandishi wa habari mkoani Kagera, likihusisha waandishi wenyewe, na wadau kutoka kada mbalimbali kama mashirika yasiyo ya kiserikali na serikali, wafanyabiashara, wanasiasa, wanafunzi na viongozi wa kidini.
Katika kongamano hilo, baadhi ya wadau wamelalamikia baadhi ya mikutano ya hadhara kuwa wagombea wamekuwa wakizungumza matusi bila kutaja sera na sifa zao stahiki, badala yake kushambulia wagombea wenzao ilhali kuna mambo ya kuzungumza, na kuwafanya wanahabari kukosa taarifa za kuandika.
Mimi ni katibu wa chama cha watu wenye ulemavu wa viungo CHAWATA Bw Switbert Mushanga,
kwakweli nasikitishwa sana na wagombea kusimama na kutukana watu badala ya sera, kwa mfano niliudhuria mkutano mmoja kata Rwamishenye, mmoja wa wagombea udiwani anasema amepanda jukwaa kumshughulikia mgombea ubunge, na kaanza kupiga mayowe, kweli inasikitisha sana.
Kaimu kamishna wa TAKUKURU mkoani Kagera Joseph Mwaiswelo, amesema kuwa muda uliobaki
waandishi wa habari wajikite katika kuelimisha jinsi ya kupiga kura kwasababu wengi hawaelewi ni namna gani wanaweza kufanya.
Kwa upande wake mwandishi habari Mac Ngaiza, amesema kuwa ni muhimu waandishi kuwajadili kwa haki
na usawa viongozi wanaogombea, kwa kueleza mambo sahihi yanayowahusu, kwasababu wananchi wanatakiwa kumjua mgombea, uwezo wake na jinsi atakavyotekeleza majukumu pindi akishaguliwa.
Kongamano la siku moja, limefanyika katika manispa ya Bukoba, kwa ufadhili wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania UTPC.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment