. Asema kazi ya kupambana na wahalifu
imeanza
. Mmoja atajwa kuchinjwa Kibeta

Wananchi wa mkoa wa Kagera wamehakikishiwa ulinzi na usalaama wakati wa maadhimisho ya siku kuu za Eid El Fitr ambazo zinatarajiwa kuadhimishwa mwishoni mwa wiki hii na Waislamu pamoja na wananchi wote nchini.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella wakati wa hafla ya kufuturisha iliyofanyika Ikulu ndongo mkoani hapa.
Amewatoa
wasiwasi wananchi wa Bukoba juu ya vitendo viovu vya kukata makoromeo wananchi
wasiyokuwa na hatia kuwa kwasasa wahalifu waliokuwa wanatekeleza vitendo hivyo
wameanza kudhitiwa na mtandao mzima tayari umekamatwa na vyombo vya ulinzi na
usalaama vinafanya kazi kuutokomeza.
Mhe.
Mongella alisema hayo mara baada ya sala ya Magharibi tarehe 15/07/2015 na
kuwasistiza waislamu wote pamoja na wananchi kuwa wasiwe na wasiwasi wowote juu
ya ulinzi na usalaama wakati wa maadhimisho hayo. Pia alisema kuwa Kamati ya
ulinzi na Usalaama imejipanga vizuri kuhakikisha maadhimisho hayo
yanaadhimishwa katika hali ya amani na utulivu.
Akishukuru
kwa niaba ya Waislamu na wanachi wengine waliohudhuria katika hafla hiyo ya
futari Sheikh wa Mkoa Aluna Kichwabuta
alimshuru Mkuu wa Mkoa wa Kagera na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
kuwakumbuka katika mfungo mtukufu wa ramadhani ambapo alisema hiyo ni ishara ya
ushirikiano na undugu wa karibu kwao na serikali.
Aidha
Sheikh Kichwabuta alikemea vitendo ambavyo vimeanza kujitokeza kwa wananchi
kuvamia vituo vya Polisi kuvichoma au kupora siraha na kuwaua Maafisa wa Polisi
ambapo alisema kuwa hiyo ni ishara mbaya na wananchi tunaanza kuhatarisha
usalama wa nchi kwa kuanza kutekeleza vitendo hivyo viovu.
Sheikh
Kichwabuta alikemea sana vitendo hivyo na kuomba sana wananchi wa mkoa wa
Kagera wasijaribu kufanya vitendo hivyo viovu bali waendelee kudumisha amani na
utulivu katika maeneo yao.
Mmoja atajwa kuchinjwa Kibeta
Wakati
mkuu huyo wa mkoa na shkh wa mkoa wakikemea na kusisitiza kuanza kwa mapambano
na wauaji, imetajwa kuwa kijana mwenye umri kati ya miaka 25-30 amechinjwa na
kunyofolewa koromeo usiku wa kuamkia leo katika kata ya Kibeta manispaa ya
Bukoba, ingawaje wiki mbili zilizopita, waziri wa mambo ya ndani Mathias
Chikawe, aliueleza mtandao huu kuwa tayari amemuagiza DCI na ameshatua Kagera
kwa uchunguzi zaidi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment