Nimeamua kuacha kuchukua fomu ya kugombea kwasababu
inaonekana wenzangu wana CCM wananitenga, tangu kata yetu ilipopoteza wenyeviti
wote wa mitaa katika uchaguzi uliopita.
Ni kauli ya mwenyekiti CCM wilaya na aliyekuwa diwani wa
kata Kashai manispaa ya Bukoba Yusuph Ngaiza, ametangaza kutogombea tena nafasi
hiyo.
Akizungumza na mwandishi habari wamtandao huu, Bwana Ngaiza
amesema kuwa ameongoza kata hiyo kwa miaka 15, ameamua apumuzike huku akiwasihi
wana CCM kuwa wamoja ili kuendeleza ushindi ulioanzishwa na waasisi hatimaye
kuwaletea wananchi maendeleo.
Ameelezea miradi ya maendeleo iliyofanywa wakati wa uongozi
wake, huku akimsihi atakayechaguliwa msimu ujao kuendeleza alichokiacha huku
akiwashukuru wa baadhi ya viongozi wa kata hiyo.
Ameongeza kuwa tayari mkandarasi anaendelea na ujenzi wa
barabara hiyo na itakamilika mwezi wa nane, hivyo akawataka wananchi kuitunza
miundombinu hiyo akisistiza viongozi wao kuendelea kupendekeza miradi kwani
Kashai bado ina uhitaji mkubwa wa maboresho.
Bwana Yusuph Ngaiza, anaendelea na nafasi yake ya uenyekiti
wa CCM wilaya alipochaguliwa katika nafasi hiyo 2012, na amesema kuwa sasa
atakuwa na nafasi nzuri kushughulikia masuala ya kisiasa kwa kuhakikisha
anasimamia viongozi watakaochaguliwa ili watekeleze ilani ya CCM.
Alianza udiwani katika kata ya Kashai mwaka 2000 kwa ushindi
wa kura 620, na mwaka 2005 aliendelea na nafasi hiyi baada ya kumshinda Khalfan
Ramadhani Bahati kwa ushindi wa kura 800 na mwaka 2010 alichaguliwa kwa
kuwashinda Ali Kabaju wa CUF , na Lenatus Kilongozi (Ikengya) wa CHADEMA,
alipowashinda kwa kura 475.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment