MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 20 May 2017

VIDEO;WALIMU 28 WAMALIZA SEMINA YAO CHINI YA UDHAMINI WA JAMBO BUKOBA


By Lameck Richard


Walimu 28 kutoka shule za msingi kumi na nne za halmashauri ya wilaya Bukoba  wamekabidhiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya semina fupi iliyoanza may 15 mwaka huu ambayo ilikuwa inaendeshwa chini ya ufadhili wa shirika la JAMBO BUKOBA.

Akikabidhi vyeti hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Bukoba,Afisa Michezo wilaya hiyo Bw,Gosbert Kamuntu amelipongeza shirika la Jambo Bukoba linaloendeshwa kwa ufadhili wa Clemens Mulokozi kwa kazi nzuri wanayoifanya huku akiwasihi wazazi na walezi kuruhusu watoto wao kushiriki michezo kwani michezo ni ajira na ni sehemu mojawapo ya kuendeleza vipaji vyao.

Kwa upande wake Meneja Mradi wa shirika la jambo Bukoba Iman Paul amesema kuwa mwaka 2008 walianza rasmi kutoa semina kwa walimu wa shule za msingi mbalimbali ndani ya manispaa ya Bukoba na halmashauri ya wilaya Bukoba ambapo kufikia may 19 mwaka huu wamekamilisha zoezi hilo kwa wilaya hizo mbili,na semina zinaendelea kutolewa kwa wilaya nyingine zote za mkoa wa Kagera .

Aidha amesema kuwa malengo ya shirika la Jambo Bukoba ni kuendeleza vipaji vya watoto kupitia michezo ndani ya mkoa wa Kagera kwa kujali usawa wa kijinsia,kutoa elimu ya ukimwi na elimu kwa ujumla.

Bi,Paul ameongeza kuwa pamoja na kuendesha michezo hiyo wamejikita pia katika kuboresha miundombinu katika shule za msingi mbalimbali ndani ya mkoa wa Kagera kujipatia kiasi cha shilingi milioni nne ambazo huzitoa kwa kila timu inayoshiriki bonanza la mkoa na ufanyika mara moja kwa mwaka.

Kwa upande wa wakufunzi katika semina hiyo mwl William Magesa na Bi,Macleth Joseph{Mrs Kamuntu}wamewasihi wahitimu wote kuhakikisha wanakuwa balozi wazuri kwa kuwafundisha wanafunzi wao  michezo yote waliyojifunza  kupitia semina hiyo .

Sanjali na hayo,wahitimu wamelipongeza shirika la jambo Bukoba kwa kuanzisha mafunzo hayo huku wakisema awali walikuwa na changamoto kubwa kimichezo lakini kuanzia sasa wanahaidi watafanya vizuri zaidi kwa wanafunzi wao kwa kuwafundisha kile walichokipata ndani ya semina hiyo.

UNAWEZA KUTAZAMA FULL VIDEO HAPA  YA MENEJA MRADI Iman Paul………….....


Na Mwanaharakati.

No comments: