MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 20 May 2017

KAULI YA KWANZA YA MUSEVEN BAADA KUKABIDHIWA UENYEKITI WA EAC




Rais wa Uganda ambaye ni mwenyekiti mpya wa Jumuhiya ya Afrika Mashariki EAC, amesema kuwa kuungana ni jambo la msingi lakini siyo kwa lengo la kuungana kusalimiana au kutakiana hali tu bali kuungana na kutekeleza mambo ya msingi na yenye kuchochea maendeleo.

Amesema hayo muda mfupi baada ya kukabidhiwa nafasi ya mwenyekiti wa jumuhiya ikulu jijini Dar es salaam Tanzania, katika kikao cha 18 cha kawaida cha EAC, ambapo imeasainiwa mikataba mbalimbali ya utekelezaji wa masuala kadhaa katika nchi sita mwanachama.

Mkutano huo umeudhuriwa na marais wawili ambao ni mwenyeji Dr. John Magufuli, Yowery Museven wa Uganda, kaimu rais wa Kenya Wiliam Rutto, na wawakilishi wengine wa marais ya mataifa ya Rwanda, Burundi, Sudan kusini na Somalia ambaye anaomba kuingizwa kwenye jumuhiya hiyo.

Rais Magufuli ambaye ameongoza jumuhiya hiyo kwa miaka miwili, amesema kuwa amefurahishwa na maendeleo ya jumuhiya hiyo, hivyo kumwomba mwenyekiti mpya kuendeleza walichoanzisha viongozi waliowatangulia, hata kama ni kazi ngumu kuendeleza jumuhiya hiyo.
 
Na Mwanaharakati.

No comments: